Kituo
cha sheria na haki za binadamu (LHRC) kimetoa ripoti ya hali ya haki za
binadamu kwa kipindi cha miezi sita kuanzia mwezi Januari hadi Juni,
2018 ambapo matukio ya ukatili kwa wanawake yameongezeka ikilinganishwa
na mwaka jana.
Akizungumza
na wanahabari Mkurugenzi mtendaji wa LHRC Anna Henga, amesema kuwa kwa
kipindi cha kuanzia Januari 2018 hadi Juni 2018, idadi ya wanawake 1,218
wameripotiwa kubakwa, inakadiriwa ni wanawake 203 kila mwezi, huku
mauaji ya kujichukulia sheria mkononi yamepungua.
“Kwa
kipindi cha kuanzia Januari 2018 hadi Juni 2018, matukio ya
kujichukulia sheria mkononi na mauaji ya kwa imani za kishirikina
yamepungua kutoka 172 hadi 106”, amesema Henga.
Henga
ameongeza kuwa hofu ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi
imeongezeka kuelekea kwenye uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2020 lakini
hakuna tukio la mauaji lililoripotiwa kuanzia Januari hadi Juni mwaka
huu.
Kwa
mujibu wa LHRC katika ripoti yake ya Mwaka 2017 wanawake walifanyiwa
aina mbalimbali za ukatili ikiwemo wa kimwili na kingono. Huku takwimu
za Jeshi la Polisi zinaonyesha kwamba jumla ya kesi za ubakaji 2,059
ziliripotiwa kufikia mwezi Machi 2017 na kufikia mwisho wa Disemba 2017,
matukio ubakaji yalikuwa 8,039, yakiongezeka kwa kiwango kikubwa
(matukio 394), ukilinganisha na matukio 7,645 ya mwaka 2016 .



No comments:
Post a Comment