Makamu
wa Rais wa Kenya, William Ruto amejibu matokeo ya utafiti uliofanywa
unaoonesha kuwa anatajwa na asilimia 33 ya Wakenya kuwa anaongoza kwa
vitendo vya rushwa.
Utafiti
huo uliofanywa na taasisi ya Ipsos Synovate, iliyopitia Kaunti 45 na
kuwahoji jumla ya watu 2,000 unamuweka Ruto kwenye nafasi ya kwanza
akiwa na silimia 33, akifuatiwa na Gavana wa Kirinyaga ambaye amepata
asilimia 31.
Kadhalika,
utafiti huo umeonesha kuwa asimilia 51 ya Wakenya wana imani na jinsi
ambavyo Rais Uhuru Kenyatta anapambana na vitendo vya rushwa.
Ruto
ameeleza kuwa utafiti huo umefanywa kama propaganda ya kumchafua
kwakuwa wapinzani wake hawawezi kushindana naye kwenye rekodi ya
kuwaletea maendeleo Wakenya.
“Wakimalizana
na propaganda zao za vichwa vya habari, tukutane kwenye kilinge cha
kuwaletea maendeleo Wakenya kwa sababu hapo ndipo ushindani wa kweli
ulipo,” alisema Ruto.
“Wapinzani
wangu wakimalizana na utafiti walioufadhili, habari za uongo, tukutane
kwenye hiki kilinge cha kuleta maendeleo kinachomlenga mwananchi wa
chini, reli ya kisasa, pato la mwananchi, barabara, kuwaunganishia
wananchi umeme, kuboresha huduma za afya na mani. Nawangojea huko,”
aliongeza.
Utafiti
huo unachukuliwa na wafuasi wa Ruto kama njia ya kutaka kukwamisha mbio
zake za kuelekea Ikulu, kwani imewekwa wazi kuwa atawania nafasi ya
urais katika uchaguzi ujao wa mwaka 2022.
Hata
hivyo, utafiti wa Ipsos haukuwaacha salama wanasiasa wengine, Daniel
Arap Moi (Rais Mstaafu), Mwai Kibaki (Rais mstaafu), Raila Odinga
(Kiongozi wa upinzani) na Rais Kenyatta wametajwa kwenye nafasi sita za
juu japo wana asilimia chache.




No comments:
Post a Comment