Na Stella Kalinga, Simiyu
Rais
Mstaafu wa Awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Benjamin William Mkapa amesema Serikali imeondoa zuio la kuuza Mazao ya
Chakula nje ya nchi ikiwa ni njia nyingine ya kuongeza soko la mazao ya
wakulima hapa nchini.
Mhe.
Mkapa amesema hayo katika Kilele cha Maonesho ya Nane nane Kitaifa
mwaka 2018 Mkoani Simiyu, Uwanja wa Nyakabindi, Halmashauri ya Mji wa
Bariadi ambapo alikuwa mgeni Rasmi akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
“Ninachukua
fursa hii kuwafahamisha kuwa Serikali imeondoa zuio la kuuza Mazao ya
Chakula nje ya nchi ikiwa ni njia nyingine ya kuongeza soko la mazao
ya wakulima hapa nchini, hata hivyo mazao hayo yatauzwa nje ya nchi kwa
kufuata sheria, kanuni na taratibu”alisema.
Aidha,
amesema Serikali inawakumbusha wananchi wote kuhifadhi akiba ya kutosha
ya chakula wakati wa kuuza mazao yao ili kujihakikishia usalama wa
chakula katika kaya zao.
Mkapa
pia amesema Serikali ina mkakati wa kuongeza uzalishaji wa zao la pamba
kutoka tani 121,000 mwaka 2016/2018 hadi kufikia tani milioni moja
mwaka 2020.
Waziri
wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba ametangaza rasmi kuwa Maonesho ya Nane
nane Kitaifa kwa miaka mitatu mfululizo hadi mwaka 2020 yatafanyika
kanda mpya Kanda ya Ziwa Mashariki katika Uwanja wa Nyakabindi Bariadi,
huku akisisitiza kuwa maonesho hayo yafanyike Kimataifa kwa
kushirikisha nchi jirani zinazoizunguka Tanzania.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka amesema Mkoa wa Simiyu
utaendelea kulipa kiupaumbele zao la Pamba na mwaka ujao uzalishaji
utaongezeka kutoka kilo milioni 70 hadi kufikia kilo 150.
“Simiyu
tunajivunia wananchi wachapa kazi wenye uthubutu na Simiyu inajengwa na
Wanasimiyu, mwaka jana tumezalisha kilo milioni 70 za pamba, kwa mwaka
huu sasa hivi msimu ukiwa umefikia katikati tuna kilo milioni 85,
mwakani tunatarajia kuzalisha kilo zaidi ya 150” alisema
Ameongeza
kuwa wananchi wamelima chakula cha kuwatosheleza si watu wa kuomba
chakula cha msaada huku akiupambanua Mkoa wa Simiyu kuwa ni mkoa pekee
ambao watu wake wanafanya biashara saa 24.
Maonesho
ya Nanenane Mwaka 2018 yaliwashindanisha wakulima na wafugaji mmoja
mmoja, Taasisi, Wakala, Mashirika ya Umma na Binafsi, Wizara pamoja na
Halmashauri 21 za Mikoa ya Simiyu Mara na Shinyanga ambapo Halmashauri
ya Wilaya ya Maswa katika Mkoa wa Simiyu imekuwa ya tatu kati ya hizo
21.
Kauli mbiu ya Maonesho ya Nanenane mwaka 2018 “ WEKEZA KATIKA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI KWA MAENDELEO YA VIWANDA”



No comments:
Post a Comment