Mbunge
wa Konde, Khatibu Saidi Haji (CUF), amemsifu Waziri wa Fedha na
Mipango, Dk. Philip Mpango kwa ‘kuyang’ang’ania’ makontena ya Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akimtaka kuyalipia kodi.
Makontena
hayo ambayo yaliingizwa Bandari ya Dar es Salaam kwa jina la mkuu huyo
wa mkoa yakidaiwa kuwa na samani za walimu wa shule mbalimbali za Mkoa
wa Dar es Salaam ambapo yalitakiwa kulipiwa kodi kwa Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA), yakitakiwa kulipiwa kodi suala lilioungwa mkono na
Waziri Mpango na kuamuru yazuiliwe hadi yatakapolipiwa kodi na
yasipolipiwa yapigwe mnada huku Rais John Magufuli akipigilia msumari wa
mwisho kumtaka Makonda ayalipie kodi makontena hayo.
Akichangia
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Ubia Baina ya Sekta ya
Umma na Sekta Binafsi (PPP), bungeni jijini Dodoma leo Jumatano Septemba
11, Haji amesema mawaziri wa aina ya Dk. Mpango ndiyo Rais Magufuli
anaowataka.
“Mheshimiwa
sheria ni msumeno na katika kutekeleza majukumu yako muhimu ya
kusimamia fedha za nchi hii hutakiwi kumwangalia usoni yeyote anayevunja
sheria za nchi hii katika kusimamia kodi za wananchi.
“Kwa
hiyo kitendo chako kitabakia katika historia, alijaribu kuwachezea
wengine lakini alichezea vyeupe amekutana na cheusi kimemtia doa, na
nakuambia Dk. Mpangio uzi ni huo huo mbane Makonda hadi mwisho ili haki
ipatikane,” amesema Khatibu.
No comments:
Post a Comment