Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
ametoa pole kwa waandishi wa habari watano wa Mkoa wa Simiyu na
Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika,Dkt. Titus Kamani waliopata
ajali katika wilayani Meatu, wakati akiwa ziarani wilayani humo, salamu
ambazo zimewasilishwa kwa niaba yake na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka, ambaye aliwatembelea katika Hospitali ya Wilaya ya Meatu
walikokuwa wakipatiwa matibabu.
Akiwasilisha
salamu za Mhe.Rais, jana jioni Mhe. Mtaka amesema magari matano ya
Simiyu ya Serikali na gari binafsi yaligongana na watu sita wakajeruhiwa
wakiwemo waandishi watano na Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya
Ushirika,Dkt. Titus Kamani na kusisitiza kuwa Mhe. Rais ameguswa na
jambo hilo, hivyo ametoa shilingi laki tano kwa kila majeruhi ili
iwasaidie katika matibabu.
“...magari
ya waandishi wa habari lakini kulikuwa na gari binafsi, baada ya
msafara wa Rais kwa sababu ya vumbi, dereva mmoja katika yale magari
alisimama kutaka kuona njia vizuri, magari yaliyokuwa yakifuatana
matano yakagongana kwa nyuma, watu sita wakapata majeraha miongoni mwao
walikuwepo waandishi wetu watano na Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya
Ushirika,Dkt. Titus Kamani”
“Mhe.
Rais anatoa salamu zake za pole kwa majeruhi wote, ameguswa sana na
jambo hili hasa pale aliposikia kuwa sehemu ya majeruhi ni waandishi
ambao tumekuwa nao pamoja katika ziara hii, wakafanya kazi kubwa ya
kuuhabarisha Watanzania, akaomba mimi kama Mkuu wa Mkoa nifikishe
salamu zake za pole kwa niaba yake kwa watu hawa sita” alisema.
Ameongeza
kuwa Mkoa utaendelea kuchukua tahadhari kupitia jeshi la polisi hasa
katika misafara ya viongozi na kuhakikisha kuwa wanajenga uelewa wa
pamoja kwa madereva wakati wa maandalizi ya safari juu ya namna ya
kuchukua tahadhari.
.Rehema
Evance ambaye ni mwandishi wa Azam TV amemshukuru Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwatambua na
kuona awape mkono wa pole ambao amebainisha kuwa fedha hizo zitawasaidia
katika kugharamia matibabu.
“
Kwanza namshukuru Mungu kwa kutujalia tukapona, lakini kipekee napenda
kumshukuru Mhe. Rais kwa kuona kuna haja ya kutusaidia katika hili, kwa
hiki alichotoa Mungu ambariki sana kitatusaidia kwenye matibabu,
tunaahidi kuendelea kuwahabarisha Watanzania na kuhakikisha yale yote
yanayotendeka ndani ya nchi yanawafikia” alisema.
Ajali
hii iliyotokea wilayani Meatu Septemba 09, 2018 imesababisha majeruhi
sita ambao ni waandishi watano Rehema Evance (AZAM TV), Belensi
China(ITV), Aidan Mhando(Channel Ten), Phaustine Fabian(Mwananchi),
Mpiga Picha Samson Masunga pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya
Ushirika,Dkt. Titus Kamani na hakuna kifo kilichotokea..
Majeruhi
wote walipatiwa matibabu katika Hospitaliya Wilaya ya Meatu ambapo
waandishi wa habari Rehema Evance (AZAM TV), Phaustine
Fabian(Mwananchi), Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika,Dkt.
Titus Kamani waliruhusiwa na Belensi China(ITV), Aidan Mhando(Channel
Ten), na Mpiga Picha Samson Masunga walipewa Rufaa kwenda Bugando kwa
uchunguzi na matibabu zaidi.
Kwa
mujibu wa majeruhi hao waliopelekwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando wote
wamefanyiwa uchunguzi na kupatiwa matibabu na Septemba 10, 2018
wameruhusiwa.
No comments:
Post a Comment