Rais
Dkt John Magufuli leo Septemba 03, 2018 atashuhudia utiaji saini wa
mkataba wa ujenzi wa meli mpya na chelezo katika Ziwa Victoria, tukio
hili linafanyika Jiji Mwanza na litarushwa moja kwa moja na TBC1, Azam Tv, ikulu.go.tz
Mikataba
hiyo itahusisha ujenzi wa meli moja mpya, chelezo ya kujenga meli hiyo,
ukarabati wa meli ya Mv Victoria na Butiama katika Bandari ya Mwanza
Kusini jijini hapa.
Meli
hiyo mpya itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 1,200 na tani 400 za mizigo
pamoja na magari madogo 20 na itafanya safari zake kati ya Mwanza na
Bukoba kupitia bandari ya Kemondo, Mwanza na Musoma na pia, Mwanza na
bandari za nchi jirani za Kenya na Uganda.
Imeelezwa
kuwa mkataba mwingine ni wa ukarabati mkubwa wa meli ya Mv Victoria
yenye uwezo wa kubeba abiria 1,200 na tani 200 za mizigo, iliyokuwa
ikifanya safari zake kati ya Mwanza na Bukoba kabla ya kusitisha mwaka
2014 kutokana na kuharibika kwa mitambo yake. Ukarabati huo unatarajiwa
kuchukua miezi 12.
Meli
nyingine itakayofanyiwa ukarabati ni MV Butiama yenye uwezo wa kubeba
abiria 200 na tani 100 za mizigo, meli ambayo ilikuwa ikifanya safari
zake kati ya Mwanza na Nansio Ukerewe kabla ya kuharibika mwaka 2010.
Kukamilika kwa meli hiyo kutarahisisha usafiri kwa wananchi waishio kwenye visiwa vya Ukerewe.
No comments:
Post a Comment