Serikali
ina mpango wa kuajiri watendaji kata 1,000 ili kupunguza pengo kubwa la
ukosefu wa watendaji hao katika maeneo mengi nchini.
Kauli hiyo imetolewa leo bungeni na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, Joseph Kandege.
Kandege
alitoa kauli hiyo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Tundulu
Kusini (CCM), Daim Mpakate ambaye alitaka kujua ni lini Serikali
itaajiri watendaji kata kwani maeneo mengi yako wazi.
Naibu
Waziri huyo alikiri watendaji ni watu muhimu katika shughuli za
maendeleo hivyo Serikali imeona umuhimu wa kuwaajiri ili kusukuma mbele
kurudumu la maendeleo.
"Tumeomba
kibali na tumepewa kuajiri watendaji kata 1,000, hivyo tuna amini
tukishaajiri hao tutakuwa tumepunguza pengo hilo kwa kiasi kikubwa,"
alisema Kandege.
Naibu Waziri huyo alisema mpango huo utafanyika mapema kwa kuwa uhitaji wao ni mkubwa.
No comments:
Post a Comment