Bodi
ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inapenda kuwataarifu
waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2018/2019 na umma kwa ujumla
kwamba imetangaza orodha ya baadhi ya waombaji mikopo ambao fomu zao za
maombi ya mikopo zina upungufu ili waweze kufanya marekebisho kwa njia
ya mtandao https://olas.heslb.go.tz kwa siku saba (7) kuanzia Jumatatu Septemba 24 hadi Jumapili Septemba 30, 2018.
Katika
kipindi hicho waombaji wote wa mikopo ambao fomu zao zina upungufu wa
baadhi ya taarifa na nyaraka zao ama za wadhamimi wao, watapaswa kusoma
majina yao kwenye orodha iliyowekwa kwenye tovuti ya HESLB www.heslb.go.tz
na kisha kuingia kwenye mtandao wa maombi ya mikopo ili kufanya
masahihisho kwa kufuata hatua zilizowekwa na baada kukamilisha,
waziwasilishe ndani ya muda uliopangwa bila kutuma kwa njia ya EMS.
Nyaraka
zote zinazokosekana ikiwa ni pamoja na vyeti vya kuzaliwa au vya vifo
vya wazazi, kurasa za taarifa na saini za mwombaji na/au mdhamini wake
zinapaswa kujazwa kwa ukamilifu, kuwa ‘scanned’ na kisha kupakiwa kwenye
mtandao baada ya kuthibitishwa na mamlaka husika.
Zoezi la Uhakiki wa Taarifa za Waombaji wa mikopo
Baada
kukamilika kwa muda wa kupokea maombi ya mikopo Julai 31, 2018, HESLB
ilikuwa imepokea jumla ya maombi 78,833 ambapo baada ya uhakiki, HESLB
ilibaini jumla ya waombaji zaidi ya 25,000 fomu zao za maombi zikiwa na
upungufu wa nyaraka na uthibitisho wa kuwezesha kuendelea na hatua
inayofuata ya kupangiwa mikopo katikati ya mwezi Oktoba, 2018.
Hitimisho
Kwa
taarifa hii pia tunapenda kuwakumbusha waombaji wa mikopo ambao wamo
katika orodha hiyo yenye upungufu wa taarifa kusoma kwa umakini na
kurekebisha kasoro hizo ili waweze kupangiwa mikopo.
Aidha
tunawatahadharisha dhidi ya matapeli wanaoweza kutumia taarifa hiyo
kuwalaghai waombaji mikopo kuwa wanaweza kuwasaidia kupata mikopo.
Tangazo maalum na mwongozo wa marekebisho vinapatikana katika tovuti ya
HESLB (www.heslb.go.tz).
Iwapo wana maswali, wawasiliane nasi kupitia:
Simu: 0736665533 au 022 5507910
Taarifa hii pia inapatikana kwenye tovuti ya HESLB www.heslb.go.tz
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mtendaji
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
Enter your comment...Makubwa
ReplyDelete