Afisa
uhamiaji katika jijini la Dodoma Edwin Mwasota amewataka wachungaji na
viongozi mbalimbali wa madhehebu ya Kikristo mkoani Dodoma kuacha tabia
ya kualika wachungaji kutoka nje ya Tanzania na kufanya mahubiri katika
jiji hilo bila kibali Maalum.
Bwana
Edwin ameyasema hayo Septemba 5 katika moja ya Ziara ya mkuu wa wilaya
ya Dodoma mjini Patrobass Katambi kwenye mikutano ya hadhara
iliyofanyika katika kata za Ipagala na Mnadani jijini Dodoma.
Afisa
Uhamiaji huyo amesema kuwa wahubiri wazawa wana uwezo wa kuhubiri hivyo
kufanya mialiko ya kualika wahubiri kutoka nje ni kujidhihisha kuwa wao
hawawezi na kubainisha kuwa katika jiji la Dodoma pamekuwepo na wimbi
la mabango ya matangazo ya wahubiri kutoka nje ya Tanzania ikiwemo Kenya
bila Uhamiaji kujulishwa juu ya ugeni huo.
"Hivi
nyie wachungaji hamjiamini kuhubiri?sasa kumeibuka wimbi la wahubiri
kutoka nje ya nchi.Ukifuatilia mtu huyo kaingiaje hapa jijini Dodoma
hauwezi kuelewa mwanzo wala mwisho.Ukienda kila mtaa hususan kwenye
nguzo za TANESCO utakuta kuna mabango ya matangazo ya Ujio wa
wahubiri
kutoka nje ya nchi mfano Kenya,Uganda.Sasa unajiuliza huko anakotoka
hakuna watu wa kuhubiriwa mpaka aje Tanzania."Alisema
Pia
Bwana Edwin aliongeza kuwa"Nimeamua kusema haya kwa sababu Nimewahi
kushuhudia mchungaji wa Kanisa Fulani kutoka nje ya nchi alikuja hapa
kwa lengo la kuhubiri ,baada ya mkutano wa mahubiri kumalizika kama
ilivyopangwa aling'ang'ania kukaa hapa nchini.Ndipo ujue kuwa Tanzania
ni kuzuri watu wanatamani Kukaa"
Aidha
Afisa huyo wa uhamiaji amewataka wananchi wa jiji la Dodoma
kushirikiana na idara ya uhamiaji kuwabaini watu wanaofanya kazi za
majumbani kutoka nje ya nchi bila kibali maalum ili hatua za kisheria
ziweze kuchukuliwa.
Alisema"Kuna
baadhi ya watanzania wamekuwa wakiwatumikisha kazi za ndani wasichana
wadogo kutoka nje ya nchi kwa kigezo cha gharama nafuu.Naomba
tushirikiane ili tuweze kuwabaini "
Kwa
upande Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya Dodoma mjini
ambaye ni mkuu wa wilaya hiyo Mhe:Patrobass Katambi amesema kuwa suala
la ulinzi na usalama ni la kila mtu hivyo jamii inapaswa kulinda mali
ya mwenzake.
"Suala la ulinzi na Usalama ni la kila mtu ,wana Dodoma tushirikiane kulinda mali ya mwenzake"Alisema .
=========================================
MWISHO.
No comments:
Post a Comment