Baada
ya bao hilo, nyuki wakaingia uwanjani jambo lililosababisha wachezaji
walale chini kwa dakika mbili, kabla ya wadudu hao kuondoka na mchezo
kuendelea.
Almanusra
Genilson Santana ‘Jaja’ aisawazishie Yanga SC dakika ya 32 baada ya
kuunganisha vizuri kwa kichwa kona ya Haruna Niyonzima, lakini Hassan
Ramadhani akauokoa ukiwa unaelekea nyavuni.
Dakika
ya kwanza tu ya kipindi cha pili, Yanga SC walipata penalti baada Salim
Mbonde kuunawa mpira kwenye eneo la hatari, lakini kipa Said Mohamed
Kasarama akapangua kwa mguu mkwaju wa Jaja.
Dakika
ya 47, Simon Msuva, aliyetokea benchi kuchukua nafasi ya Hamisi Kiiza
‘Diego’aliifungia Yanga SC bao, lakini refa akasema aliotea. Dakika ya
49 tena, Mrisho Ngassa alifunga bao lakini refa akasema aliotea pia.
Dakika
ya 67, Simon Msuva alivamia langoni mwa Mtibwa na kutoa vitu
vilivyokuwa chini upande wa nyavu kubwa na kukimbia navyo huku
akikimbizwa na kipa Said Mohamed Kasarama kabla ya kuvitupa nje.
Dakika
ya 82 mpishi wa bao la kwanza, Ame Ali aliifungia Mtibwa bao la pili
baada ya kufanikiwa kuwahadaa mabeki wawili wa kati wa Yanga SC, Nadir
Haroub ‘Cannaaro’ na Kevin Yondan kisha kumtungua Dida kufuatia pasi
nzuri ya Hassan Ramadhani.
Yanga
SC iliathiriwa na mabadiliko iliyoyafanya dakika za mwishoni kumtoa
Mbuyu Twite aliyekuwa mhimili wa safu ya ulinzi na kuingiza
mshambuliaji, Said Bahanuzi.
Kocha
wa Yanga SC, Marcio Maximo ambaye alimfundisha kocha wa Mtibwa Sugar,
Mecky Mexime alipokuwa Taifa Stars alikuwa mnyonge baada ya meci hiyo.
Kikosi
cha Mtibwa Sugar kilikuwa; Said Mohammed, Hassan Ramadhani, David
Luhende/Majaliwa Shaaban dk64, Salim Mbonde, Andrew Vincent, Shaaban
Nditi, Ali Shomary, Muzamil Yassin, Ame Ali, Mussa Mgosi/Vincent
Barnabas dk50 na Mussa Nampaka/Dickson Daud dk72.
Yanga
SC; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua/Omega Seme, Nadir
Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Mbuyu Twite/Said Bahanuzi dk72, Hassan
Dilunga, Haruna Niyonzima, Genilson Santana ‘Jaja’, Mrisho Ngassa na
Hamisi Kiiza/Simon Msuva dk46.
|
Shujaa; Didier Kavumbangu akishangilia baada ya kuifungia Azam FC mabao mawili katika ushindi wa 3-1
Beki
Aggrey Morris akaipatia bao la pili Azam FC dakika ya 23 aliyemalizia
mpira wa adhabu uliopigwa na Kipre Tchetche kufuatia beki Gardiel
Michael kuchezewa rafu na Bantu Admin.
Baada
ya mabao hayo mawili ya haraka haraka, kocha wa Polisi Morogoro,
Mohammed Adolph ‘Rishard’ alimpumzisha kiungo Bantu Admin na kumuingiza
James Mganda.
Mabadiliko
hayo kidogo yaliituliza Polisi na kuanza kufika kwenye lango la Azam,
ingawa hawakufanikiwa kupata bao hadi dakika 45 za kwanza
zilipokamilika.
Mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Danny Mrwanda alidhibitiwa vikali na mabeki wa Azam leo.
Kipindi
cha pili, Azam FC ilirudi vizuri na kusukuma mashambulizi mfululizo
langoni mwa Polisi, lakini mshambuliaji Kipre Tchetche alikosa mabao
matatu ya wazi.
Nahoda
Bakari aliipatia bao Polisi dakika ya 60 baada ya kuanzishiwa kona fupi
na kumtungua kwa shuti la umbali 22 kipa Aishi Manula.
Didier Kavumbangu aliifungia bao la tatu Azam FC dakika ya 90 akimalizia krosi ya Farid Malik.
Kikosi
cha Azam FC kilikuwa; Aishi Manula, Shomary Kapombe, Gardiel Michael,
David Mwantika, Aggrey Morris, Kipre Balou, Himid Mao/Khamis Mcha
‘Vialli’ dk72, Mudathir Yahya, Didier Kavumbangu, Kipre Tchetche/Farid
Malik dk72 na Salum Abubakar.
Polisi
Moro; Tony Kavishe, Rogeri Fred, Simon Fanuel, Ally Feruzi Telu,
Lulanga Mapunda, Said Jella, Bantu Admin/James Mganda dk22, Nahoda
Bakari/Suleiman Kassim ‘Selembe’ dk65, Danny Mrwanda, Machaku Salum na
Nicholas Kabipe/Edgar Charles dk65.
|
|
|
No comments:
Post a Comment