KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

June 3, 2016

TAARIFA YA UDAHILI KATIKA VYUO VYA MAENDELEO YA JAMII

index
Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ina vyuo tisa (9) vinavyotoa mafunzo ya taaluma ya Maendeleo ya Jamii katika ngazi ya Cheti, “Diploma”, “Degree” na  “Postgraduate Diploma” kama ifuatavyo:-
  • Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru iliyoko Wilaya ya Arumeru, Mkoani Arusha, inatoa Shahada (Degree). katika fani ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Maendeleo na  Upangaji na Uendeshaji Shirikishi wa Miradi.  Aidha, Taasisi hiyo pia inatoa Stashahada ya  Uzamili (Postgraduate Diploma) katika Maendeleo ya Jamii.
  • Vyuo vya Maendeleo ya Jamii Ufundi Missungwi (Mwanza) na Mabughai (Lushoto) vinatoa Kozi ya Maendeleo ya Jamii Ufundi, kuanzia  ngazi  ya Cheti hadi Diploma.
  • Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare kilichopo Wilaya ya Musoma Mkoani Mara, kinatoa mafunzo ya Maendeleo ya Jamii kuanzia ngazi ya Cheti hadi Diploma.
  • Vyuo vya Maendeleo ya Jamii Rungemba (Mafinga – Mufindi) na Monduli (Arusha) vinatoa mafunzo ya Taaluma ya Maendeleo ya Jamii katika ngazi ya Diploma.
  • Vyuo vya Maendeleo ya Jamii Ruaha (Iringa), Uyole (Mbeya) na Mlale (Songea) vinatoa mafunzo ya Maendeleo ya Jamii katika ngazi Cheti.
  • Madhumuni ya Vyuo vya Mendeleo ya Jamii:
Madhumuni ya vyuo hivi  ni pamoja na:
  1. Kutoa mafunzo ya taaluma ya Maendeleo ya Jamii kwa wahitimu wa kidato cha nne na sita waliotoka shuleni moja kwa moja.
  2. Kuendeleza Maafisa Maendeleo ya Jamii walioko kazini wenye taaluma ya Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Jamii;
  • Kupata wataalamu mahiri wa Maendeleo ya Jamii wenye uwezo wa kuiwezesha jamii kujiletea maendeleo yao wenyewe.
  1. Kuandaa mitaala inayokidhi mahitaji ya taaluma ya maendeleo ya jamii sanjari na mabadiliko yanayotokana na utandawazi, soko la ajira pamoja na sayansi na teknolojia.
  • UTOAJI WA TAALUMA YA MAENDELEO YA JAMII


Taaluma ya Maendeleo ya Jamii inatolewa  kwa kuzingatia taratibu na kanuni zinazotolewa na kusimamiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE).  Hivyo NACTE inasimamia uandaaji wa mitaala inayotumika katika utoaji wa mafunzo, muda wa masomo, mitihani na vigezo vyake, pamoja na ubora wa vyeti wanavyotunukiwa wahitimu kwa kila ngazi.
  • Mafanikio katika VYUO VYA MAENDELEO YA JAMII
Vyuo vya Maendeleo ya Jamii vimepata mafanikio mbalimbali katika utekelezaji wa majukumu yake, mafanikio hayo ni pamoja na:
  1. Udahili wa wanachuo kuongezeka kutoka wanachuo 940 (wanawake 513 na Wanaume 427) mwaka 2005 hadi kufikia wanachuo 3,634 (wanawake 2,407 na wanaume 1,227) mwaka 2014, kwa lengo la kuongeza wataalamu wa maendeleo ya jamii ambao ni muhimu katika Kuraghbisha jamii kushiriki katika shughuli za maendeleo. 
  2. Jumla ya Wanachuo 13,332 walihitimu katika Taaluma ya Maendeleo ya Jamii kutoka katika Vyuo tisa vya Maendeleo ya Jamii na kuwezesha kuongeza idadi ya Maafisa Maendeleo ya Jamii walioajiriwa katika Halmashauri kutoka Maafisa 1,855 mwaka 2005 hadi kufikia Maafisa 2,675 mwezi Machi, 2014 ikiwa ni ongezeko la asilimia 44.
  • Kupanda hadhi ya kitaaluma ya Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru hadi kuwa Taasisi ya Elimu ya Juu inayojitegemea kiutendaji,
  1. Kuwezesha Vyuo vya Maendeleo ya Jamii kusajiliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) na kutambuliwa katika ngazi tofauti;
  2. Kutoa mafunzo ya Cheti, Diploma na Degree katika Maendeleo ya Jamii kwa ufanisi;
  3. Kuwa na wakufunzi mahiri wenye weledi katika taaluma ya maendeleo ya Jamii.
  • Kutoa wahitimu wanaokidhi soko la ajira kutokana na umahiri na uzoefu katika fani ya maendeleo ya jamii.
  • Aidha, vyuo vinapanua wigo wa utoaji wa taaluma ya Maendeleo ya Jamii kwa kutekeleza majukumu yake makuu ambayo ni mafunzo, utafiti na ushauri elekezi.
Ndugu Waandishi wa Habari,
Wizara inawataarifu wahitimu wa Kidato cha NNE na Kidato cha SITA wenye utashi katika fani ya maendeleo ya jamii waweze kutuma maombi yao kwenye “Central Admission System” (CAS), kupitia www.nacte.go.tz.
Katika kuchochea ari na mwamko wa wananchi kutumia rasilimali zinazowazunguka na kushiriki kikamilifu katika kujiletea maendeleo yao, ni muhimu kwa Halmashauri, Majiji, Miji, Manispaa na Wilaya, kutoa kipaumbele katika kuwaajiri Maafisa Maendeleo ya Jamii  ambao wanajukumu la kuhamasisha uzingatiwaji wa dhana ya maendeleo ya jamii ambayo inajenga na kuimarisha misingi ya watu katika jamii kujitambua, kuainisha vipaumbele, kubaini fursa na kuondoa vikwazo vya maendeleo.
Imetolewa na – Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto

No comments:

Post a Comment