KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

October 25, 2014

BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI LASIMAMA, KISA MPAKA SHYROSE AJADILIWE KWANZA

Shyrose
photo
Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki  Angela Kizigha (kushoto) na  Abubakar Zein wkishauriana kabla ya Bunge hilo kuahirishwa jana.     

MTANDAO wa The News Times wa Rwanda unasema kwamba  wiki ya kwanza ya Bunge la Afrika Mashariki (EALA)  linalokutana Rwanda imekuwa ya kuahirisha ahirisha vikao kutokana na wabunge kutaka awajibishwe kwanza Shyrose Bhanji Mbunge kutoka Tanzania kutokana na utovu wa nidhamu.

Baadhi ya Wabunge walisema jana kwamba hakuna kazi itakayofanyika Bungeni humo mpaka Shyrose ajadiliwe kwanza.Wabunge wanamlaumu Spika  Margret Nantongo Zziwa kwa kumbeba Shyrose .

 Hili ni sakata jipya miongoni mwa vioja vinalolikumba Bunge hilo.
Hivi karibuni lilipangwa kufanya vikao vyake Dar es Salaam, lakini likaahirishwa kutokana na akidi kutotimia.Ikumbukwe pia mwezi June mwaka huu,wabunge walijaribu kutaka kumg'oa Spika kwa madai ya kutoridhishwa na kiwango chake cha utendaji wa kazi na pia matumizi mabaya ya ofisi.

Baadhi ya madai ambayo yamesambazwa kwenye mitandao juu ya Shyrose ni  kushinikiza Shy-Rose awajibishwe, huku wakitaka pia Spika wa Bunge hilo hilo pia kujiuzulu.

Chanzo kinasema kuwa
kwamba tarehe 8 mwezi huu wakati wabunge wa bunge hilo wanakwenda Brussels ,nchini Ubeligiji kwenye Bunge la Ulaya Syrose alikunywa pombe kupita kiasi na kwamba alikuwa akiwatukana wafanyakazi wa ndege.

Chanzo kinadai aliwaambia wafanyakazi hao kuwa  hawajuwi kuwa yeye yeye ni mbunge wa EAC? Akaanza kufanya fujo ndani ya ndege, akachukua chupa akapasua! Inadaiwa kuwa watu wa usalama ndani ya ndege wakamkamata na kumtia pingu! 

Habari hizo zinadai kuwa Pilot alikataa kuendelea na safari akataka kushusha ndege Cairo. Walimsihi sana Pilot ndio akakubali kwa masharti Shyrose adhibitiwe!

Baadhi ya Wabunge wenzake wanadai kuwa walipoifika Brussels vioja havikuisha na kwamba aliendelea kuwasakama.

Akizungumza na Blog hii kutoka Kigali,Shyrose alikana madai hayo na kusema ni njama za wabunge kutoka nchi mmoja mwanachama kwa kile alichokieleza kumtetea Spika wa Bunge hilo.

“Si unakumbuka Spika alikuwa ang’oke,mimi nikasimama kidete kumtetea, sasa wananipakazia ili kunichafua mbele ya umma,”

Alisema Wabunge hao wanataka Spika ang'oke ili wapenyeze ajenda zao kiulaini na kwamba nchi zao zimekuwa zikiitenga Tanzania katika mambo mbalimbali.

Alisema kuwa maneno yote hayo ni ya kutunga na kwamba hakunywa pombe kupita kiasi na kama angefanya hivyo wenye ndege wangechukua hatua kali dhidi yake.

Anadai kusakamwa kwake pia kunatokana na yeye kuyapigania maslahi ya Tanzania ndani ya Bunge hilo kwani baadhi ya wabunge wanachama wamekuwa na ajenda zao za siri dhidi ya Tanzania.

 


No comments:

Post a Comment