KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

October 21, 2014

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA, AWAONGOZA WAOMBOLEZAJI KUUAGA MWILI WA ALIYEKUWA AFISA MNADHIMU MKUU MSAIDIZI WA JESHI LA MAGEREZA

image
Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(suti nyeusi), akiwa amesimama wakati mwili wa aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkuu Msaidizi wa Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Stephen Nzawila, ulipowasili tayari kwa kuuagwa rasmi nyumbani kwake Ukonga, Dar es Salaam jana Oktoba 20, 2014. Wa kwanza kushoto ni Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Nicas Banzi, wa pili kushoto ni Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Jumanne Mangara, wa kwanza kulia ni Kamishna wa Fedha na Utawala, Gaston Sanga, wa pili kulia ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.
m1 
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja, akisaini katika kitabu cha Maombolezo nyumbani kwa aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkuu Msaidizi wa Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Stephen Nzawila ambaye amefariki Jumapili tarehe 19 Oktoba, 2014 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Jijini Dar es Salaam.
  image_1
Mchungaji wa Kanisa la Moravian, lililopo Ukonga Banana Relini, Hansi Mwakijoja, akiwaongoza waombolezaji kwa sala kabla ya kuuaga rasmi mwili wa aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkuu Msaidizi wa Jeshi la Magereza.
  image_2
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja, akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkuu Msaidizi wa Jeshi la Magereza.
image_3
Baadhi ya Maofisa na Askari wa Jeshi la Magereza, wakiwa wamejipanga katika mstari tayari kuuaga mwili wa aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkuu Msaidizi wa Jeshi la Magereza jana Oktoba 20, 2014 Ukonga, Jijini Dar es Salaam. Mwili wa Marehemu unatarajiwa kusafirishwa leo kuelekea Tutuo Wilayani Sikonge, Mkoani Tabora kwa Mazishi.
  image_4
Mke wa Aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkuu Msaidizi wa Jeshi la Magereza, akiwa na majonzi makubwa na waombolezaji kabla ya kuuaga rasmi mwili wa  mume wake.
image_5
Sehemu ya Waombolezaji waliojitokeza kuuaga mwili wa aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkuu Msaidizi wa Jeshi la Magereza, wakisikiliza kwa makini wasifu wa Marehemu kabla ya kuuaga rasmi.
image_6
Bendi ya Jeshi la Magereza, ikitumbuiza katika hafla fupi ya kuuaga mwili wa aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkuu Msaidizi wa Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Stephen Nzawila.
  m2 
Mwili wa aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkuu Msaidizi wa Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Stephen Nzawila ukiwa umebebwa na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza kabla ya kuagwa rasmi leo Oktoba 20, 2014 nyumbani kwake, Ukonga Dar es Salaam.
(Picha na Lucas Mboje, wa Jeshi la Magereza).

No comments:

Post a Comment