Rais
Dkt. Jakaya Kikwete, akiangalia ramani ya Tanzania inayoonyesha mchoro
wa reli ya Kati, inayotarajiwa kujengwa upya na kwa viwango vya kisasa,
wakati alipokutana na uongozi wa juu wa makampuni ya China yakiongozwa
na China Railway Group Ltd. Makampuni mengine ni SINOSURE, Exim Bank,
China Development Bank na China Agriculture Development Bank. Rais Dkt.
Kikwete yuko nchini China kwa ziara rasmi ya kikazi (State Visit).
Rais Dkt. Jakaya Kikwete, akifanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni
ya China Railway Group Limited, Bw. Li Changjin, na msafara wake kuhusu
mpango wa serikali ya Tanzania wa kujenga reli mpya na ya viwango vya
kisasa kutoka Dar Es Salaam hadi Kigoma, Tabora kwenda Mwanza, Kaliua
kwenda Mpanda hadi Ziwa Tanganyika. Mazungumzo hayo yamefanyika huko
Beijing tarehe 24.10.2014.
No comments:
Post a Comment