SERIKALI kupitia Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limemtaka Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama kuongeza ufanisi zaidi
katika Tamasha la Krismasi mwaka huu kwa sababu kupitia matamasha yake
anafanikisha matakwa ya jamii yenye uhitaji maalum
Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mungereza alisema kwa mwenendo huo bora unaofanywa na Msama anatoa wito kuendeleza mwenendo huo ili kuisaidia jamii. Mungereza alisema Msama anafanikisha hayo kwa sababu anaipenda jamii ambako alitoa wito kwa wadau wa muziki wa Injili kujitokeza kwa wingi katika tamasha hilo linalotarajia kuanza Desemba 25 hapa nchini ili kufikia malengo stahili.
Katibu huyo alisema mbali ya kuchangia
jamii pia kupitia tamasha hilo wananchi wa maeneo husika wanapata
fursa nyingi katika maeneo yao kama madereva bodaboda, texi na biashara
nyingine. “Wananchi wa mikoa itakayofikiwa na tamasha hilo watambue
kwamba ni lao, hivyo wajitokeze kwa wingi kwani viingilio
vitakavyopatikana vinasaidia wenye uhitaji maalum kama yatima, wajane,
walemavu na wengineo,” alisema Mungereza.
Kuhusu waimbaji, Mungereza
alisema waichukulie sanaa kwamba ni kazi watumie vipaji vyao hasa
wakifikiria jamii kwani wanahitajika kutoa elimu ya uraia kutoka
kwao. Katika hatua nyingine, Kampuni ya Msama imepokea kibali cha
kufanikisha Tamasha la Krismasi mwaka huu ambako kampuni hiyo
imejipanga kufanya tamasha hilo katika baadhi ya mikoa hapa
nchini.
Naye mmoja wa Watendaji wa Kampuni ya Msama, Jimmy Rwehumbiza
aliyepokea kibali cha Tamasha la Kriamsi aliishukuru Basata kwa
kufanikisha kibali sambamba na kupokea ushauri na mapendekezo
yanayotolewa mara kwa mara yanayofanikisha matamasha hayo.
No comments:
Post a Comment