Hatimaye
mbivu na mbichi leo zimejulikana baada ya vigogo walioshiriki kugawana
fedha za Escrow kupitia Benki ya Mkombozi kutaja Bungeni leo, waliotajwa
kulamba ngawila hizo ni Andrew Chenge bilioni 1.6 Profesa Muhongo
ambaye ni Waziri wa Nishati na Madini 1.6 bilioni, Profesa Anna Tibaijuka bilioni
1.6 na Askofu Method Kilani milioni 80 na Mchungaji mmoja milioni
40.
Mbunge wa Sengerema naye alinyaka milioni 40.
Kamati hiyo imependekeza pia Waziri Mkuu ajiuzuru na pia Bodi ya
Tanesco ivunjwe na ichukuliwe hatua za kisheria. Wengine ni Katibu Mkuu
wa Wizara ya Nishati na Madini naye awajibishwe. Kamati ya Zitto pia
imemlaumu Waziri Mkuu kipekee kwa kulipotosha bunge na umma kwa ujumla
kwamba dili hilo lilikuwa halali.
Kesho Serikali itapewa muda wa kujibu hoja hilo kabla ya wabunge hawajanza kuchangia.
No comments:
Post a Comment