Kamishna
wa Madini Tanzania, Mhandisi Paul Masanja (katikati) akisisitiza jambo
wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa madini ya Shaba. Wengine
kutoka kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania
(TMAA) Mhandisi Dominick Rwekaza, Kamishna Msaidizi wa Madini na Ukaguzi
wa Migodi, Ally Samaje, Kaimu Kamishna Msaidizi sehemu ya Uongezaji
Thamani Madini, Latifa Mtoro na Mwakilishi wa Chama cha Wachimbaji
Wadogo wa Madini (FEMATA), John Mvumula.
Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Paul Masanja (katikati) katika
picha ya pamoja na washiriki wa mkutano wa wadau wa madini ya Shaba
ambao umewajumuisha wafanyabiashara wa madini ya Shaba, wachimbaji
wadogo, viwanda vya kuyeyusha madini ya Shaba, Makamishna Wasaidizi wa
Madini kutoka Kanda mbalimbali nchini pamoja na baadhi ya Maafisa Madini
Wakaazi. Mfanyabiashara wa madini ya Shaba kutoka Kanda ya Kati Doreen Kisia, akisistiza jambo wakati akichangia hoja katika mkutano huo.
Kamishna
Msaidizi Kamishna Msaidizi wa Madini na Ukaguzi wa Migodi, Ally
Samaje, akisalimiana na baadhi ya wadau wa madini ya Shaba waliohudhuria
mkutano huo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) Mhandisi Dominick Rwekaza, (kulia) akiongea jambo wakati wa mkutano huo
………………………………………………………………………….
Na Asteria Muhozya, Dare s Salaam
Wizara ya Nishati na Madini imekutana na wadau wa madini ya
Shaba katika mkutano wa siku mbili ulioanza tarehe 24- 25 Novemba, 2014
na kuwashirikisha wafanyabiashara wa madini hayo, wachimbaji wadogo,
viwanda vya kuyeyusha madini ya Shaba, Makamishana Wasaidizi wa Madini
kutoka Kanda mbalimbali nchini pamoja na baadhi ya Maafisa Madini
Wakaazi.
Akifungua mkutano huo, unaolenga kujadili masuala mbalimbali
yanayohusu sekta ndogo ya madini ya Shaba na namna ya kuyaongezea
thamani madini hayo, Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Paul Masanja
amewataka wachimbaji wadogo nchini kutumia fursa zinazotolewa na Wizara
ya Nishati na Madini ikiwemo kupata ruzuku ili waweze kuendeleza
shughuli za uchimbaji wa madini jambo ambalo litasaidia kuyaongezea
thamani madini hayo.
Aidha, Kamishna Masanja ametumia fursa hiyo, kuwataka wachimbaji
na wafanyabiashara kuacha kufanya biashara kinyume na sheria na
taratibu kwa kuwa jambo hilo linaikosesha Serikali mapato ikiwemo
kuchangia madini hayo kutokupata thamani halisi.
Vilevile Kamishna Masanja ameeleza kuwa, Serikali itaendelea
kuzuia usafirishaji madini ghafi ya Shaba na kueleza kuwa, “Haturuhusu
madini ghafi ya shaba kutoka nje, tunataka yatoke yakiwa tayari ni
madini, kwasababu kuna zaidi ya shaba hivyo tunapoteza, tunataka
kuyaongeza thamani madini yetu hapa hapa nchini”, alisisitiza Masanja.
No comments:
Post a Comment