View the slide show
KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668
www.utt-pid.org
TEMBELEA: www.utt-pid.org
December 24, 2014
RAIS DK. SHEIN ATOA VIFAA VYA MCHEZO WA RIADHA IKULU
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akikabidhi vifaa vya Riadha kwa Mwenyekiti wa mchezo huo Wilaya ya Kaskazini B Unguja Juma Hassan Ali wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa mbali mbali vya Riadha katika Wilaya ya kumi za Unguja na Pemba leo Ikulu Mjini Unguja.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Sherry Khamis akionesha baadhi ya Vifaa vya Riadha kwa Viongozi wa Mchezo huo walipofika Ikulu Mjini Unguja kuonana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)kwa mazungumzo na hatimae kuwakabidhi vifaa hivyo alivyovitoa katika kumarisha Mchezo huo hapa Zanzibar,
Vifaa vya Mchezo wa Riadha vikiwa katika utaratibu uliopangwa ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alivigawa kwa wawakilishi wa Mchezo huo katika Wilaya ya kumi za Unguja na Pemba katika hatua zake za kuupa nguvu mchezo huo ikiwemo na michezo mbali mbali hafla ya kukabidhi vifaa hivi ilifanyika ikulu Mjini Unguja leo,[Picha na Ikulu.]
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment