![]() |
| Prof.Muhongo Dar es Salaam. Zikiwa zimebaki siku tatu kabla ya Bunge la Jamhuri ya Muungano kuanza mjini Dodoma, sasa hakuna shaka kwamba Rais Jakaya Kikwete atafanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri wakati wowote kuanzia leo na kabla ya Jumapili (saa 48) kutokana na kukabiliwa na safari ya nje. Rais anatarajiwa kufanya mabadiliko hayo baada ya kumwondoa Anna Tibaijuka, ambaye alikuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kuhusishwa na kashfa ya uchotwaji fedha kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow baada ya kuingiziwa Sh1.6 bilioni kwenye akaunti yake.
Mwingine ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo, ambaye anatuhumiwa kutoshughulikia kwa makini sakata
hilo na kusababisha Serikali kupoteza fedha hivyo kuwapo kwa uwezekano
mkubwa wa kumvua uwaziri utakaomlazimu Rais kufanya mabadiliko madogo
kwenye baraza lake, ikiwa ni miezi isiyozidi mitano kabla ya kuvunja
Bunge kupisha Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.
Habari ambazo Mwananchi imezipata zinaeleza kuwa Rais Kikwete anaweza kutangaza mabadiliko hayo wakati wowote kuanzia leo.
“Rais anaondoka Jumapili kwenda Davos (Uswisi
kuhudhuria mkutano wa Jukwaa la Kiuchumi la Dunia (WEF)), hivyo kwa
jinsi yoyote ile ni lazima atangaze baraza kesho (leo) au Jumamosi,”
alisema mpashaji habari wetu.CHANZO MWANANCHI
|
January 23, 2015
HATMA YA MUHONGO KUJULIKANA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment