KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

January 25, 2015

HII NZURI, EWURA KUSHUSHA BEI YA UMEME

Wakala wa Udhibiti na Usimamizi wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), umetangaza kuwa wakati wowote kuanzia sasa serikali itapunguza bei ya umeme  baada ya gharama za  mafuta kupungua katika soko la dunia.
Tanesco inauza  'uniti' moja ya umeme kwa Shilingi 306 na pia hutoza  tozo la Shilingi 7,000 ambalo halina kuhojiwa wala kupingwa likidaiwa ni la  kuendesha shughuli za Ewura, Wakala wa Umeme Vijijini (REA) na kodi ya VAT.

Kaimu Mkurugenzi wa Umeme wa Ewura, Godfrey Chibulunje, alisema wakati wa mkutano wa wadau wakiwamo viongozi vya vyama vya siasa visivyo na wabunge.

Alitoa ufafanuzi huo baada ya viongozi hao kuwabana wataalamu hao na watendaji wa wakala huyo, Shirika la Umeme la Tanesco kueleza kwa nini hawashushi bei za umeme wakati mafuta yameshuka.

Aidha, Chibulunje alisema serikali ipo katika mchakato wa kupitia mwenendo wa kupungua kwa bei ya mafuta kwa lengo la kuangalia namna ya kuwapunguzia mzigo wananchi.

‘’Muda si mrefu wananchi wataona matokeo ya kuanguka kwa bei ya mafuta, tunachokifanya ni kupitia gharama ya ununuzi wa mafuta mazito na kiasi gani wananchi wanaweza kuondokana na mzigo wa kununua umeme,” alisema.

Walihoji pia sababu za kuuza umeme ghali wakati kampuni binafsi ya  kuzalisha umeme ya IPTL imeshusha bei. Chibulunje alisema hana  taarifa kuwa IPTL imepunguza bei ya  umeme inaouza  Tanesco.

 “Kama serikali tulisikia taarifa hizo kwenye vyombo vya habari, tunachojua IPTL inauza umeme kwa bei ya zamani, hizo taarifa ya kushusha hatuna na kama zipo hazijatufikia kiofisi,” alisema Chibulunje.

Alifafanua kwamba kiutaratibu kama kampuni au shirika linataka kupunguza au kupandisha bei ya huduma lazima inawasilisha mapendekezo ofisini kwake kwa ajili ya kufanyia kazi, hata hivyo haikufanyika jambo kama hilo.

Awali, Mwenyekiti wa makatibu wa vyama 12 vilivyoshiriki katika mkutano  huo, Ali Kaniki, alisema wanasikitishwa na hali ya wananchi kuendelea kuteseka na kubebeshwa gharama kubwa ya huduma hiyo wakati kuna baadhi ya kampuni zimeanza kushusha bei ya umeme.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments:

Post a Comment