KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

January 21, 2015

IKULU:SIKU ZA MUHONGO ZINAHESABIKA

prof muhongo
Aziza Masoud na Grace Shitundu, Dar es Salaam
IKULU imewataka Watanzania kuwa na subira kwa kuwa Rais Jakaya Kikwete wakati wowote kuanzia sasa atatoa uamuzi dhidi ya tuhuma zinazomkabili Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
Profesa Muhongo na baadhi ya viongozi wengine wa Serikali wanahusishwa na sakata la uchotwaji wa zaidi ya Sh bilioni 300 kwenye akaunti ya Tegeta Escrow.
Viongozi wengine ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Eliakim Maswi ambaye amesimamishwa kupisha uchunguzi, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema ambaye amejiuzulu na aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka ambaye tayari uteuzi wake umetenguliwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salvatory Rweyemamu, alisema si kweli Rais Kikwete anakwepa kumwajibisha Profesa Muhongo kama watu wengi wanavyodai.
Alisema kinachofanywa na Rais Kikwete ni kufuata utaratibu unaotakiwa.
“Siku mbili tatu alizosema rais maana yake ni hivi karibuni na msidhani anakimbia kutoa uamuzi… siku si lazima zihesabike, ni siku yoyote atatoa majibu.
“Tena nawaambia msikomalie suala hili kama vile ni la kufa na kupona, rais atalifanyia kazi muda si mrefu,” alisema Salva.CREDIT;MTANZANIA

No comments:

Post a Comment