![]() |
| Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga SCP Charles Mkumbo akionesha nguo ambazo zilikutwa kwa Mtuhumiwa kiongozi huyo wa genge la uhalifu ambazo zinasemekana ni za baadhi ya watu waliouawa wakiwemo majambazi aliokuwa akishirikiana nao ambao aliwauwa kwa maslahi yake. |
![]() |
| Sehemu ya vitu vilivyokutwa kwa mtuhumiwa huyo. |
Kamanda
wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza,SACP Valentino Mlowola akiwa na
makamanda wenzake SACP Charles Mkumbo (Shinyanga) na SACP Justus
Kamugisha (Simiyu) wakati wakizungumza na waandishi wa habari kufuatia
kutiwa mbaroni kwa mtuhumiwa wa ujambazi ambaye pia ni mfanyabiashara
aitwaye Njile Samweli (46) marufu kwa “John” wa mjini Bariadi mkoani
Simiyu, aliyekuwa akifanya matukio ya uhalifu katika Mikoa ya Mwanza,
Simiyu, Shinyanga, Singida na Tabora.
Kamanda
wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga,SACP Charles Mkumbo akionesha
silaha iliyokuwa ikitumiwa katika harakati za matukio ya ujambazi katika
kijiji cha Idukilo Kata ya Luhumbo Mwadui wilayani Kishapu Mkoa wa
Shinyanga.Kushoto ni Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza,SACP
Valentino Mlowola na kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu,SACP
Justus Kamugisha.




No comments:
Post a Comment