![]() |
| Ongwen kulia akiwa na kamanda mkuu wa kikosi cha Afrika kinachomsaka mkuu wa kundi la LRA Joseph Kony |
Kamanda mkuu wa kundi la waasi la
LRA nchini Uganda Dominic Ongwen amewasili mjini Hague ambako
atafunguliwa mashitaka ya uhalifu wa kivita.
Ongwen, alikuwa
kamanda mwenye kuogopewa sana katika kundi la waasi la LRA na alikamatwa
katika Jamhuri ya Afrika ya Kati mapema mwezi huu.
Uganda
ilikubali kwamba muasi huyo apelekwe katika mahakama ya kimataifa ya
ICC, licha ya nchi hio kuwa mkosoaji mkubwa wa mahakama hio.
Wanajeshi wa Marekani wakishirikiana na wa Afrika, wamekuwa wakifanya msako dhidi ya Ongwen tangu mwaka 2011.
Anasemekana kua naibu wa kiongozi wa LRA Joseph Kony ambaye bado yupo mbioni.
ICC ilisema kwamba Ongwen atazuiliwa katika kituo kimoja nchini Uholanzi hadi mahakama itakapokuwa tayari kusikiliza kesi yake.
Alitarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu alipowasili Hague huku tarehe ya kusikilizwa kwa kesi yake ikisubiriwa.
Taarifa
ilitolewa na Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na katibu
mkuu wa umoja huo ikipongeza hatua ya kumpeleka Ongwen mjini Hague.
Ban alisema ni hatua kubwa katika kuhakikisha kwamba waaathiriwa wa unyama uliotendwa na LRA wanapata haki.



No comments:
Post a Comment