Mwanamume
mmoja mwenye asili ya nchini Mali ambaye aliwaficha wauza maduka katika
duka kubwa maarufu kama supermarket mjini Paris wakati wa shambulio la
kigaidi lililotekelezwa na watu wanaodhaniwa wapiganaji wa kiislamu
amepewa hati halali ya ukaazi na kuwa raia halali wa Ufaransa.
Kwa
pamoja waziri mkuu wa Ufaransa Manuel Valls na waziri wa mambo ya ndani
Bernard Cazeneuve walizungumza katika karamu ya kumpongeza na
kumshukuru Lassana Bathily kwa ushujaa wake kwa niaba ya taifa lake .
Kijana
huyo ana umri wa miaka ishirini na minne, na kazi aifanyayo ni muuzaji
msaidizi katika supermarket hiyo,ambaye alifanya kazi kubwa ya
kuwaongoza na kuwaficha katika eneo la juu la chumba baridi cha
kuhifadhia bidhaa na kisha akazima taa za duka hilo kubwa ,kisha
akawapigia polisi simu kwa msaada wakati walipovamiwa.
Baada ya
tukio hilo, likapitishwa azimio aitwe apewe uraia wa nchi hiyo ya
Ufaransa ,hata hivyo inaelezwa kwamba Bathily ameishi nchini humo kwa
miaka tisa sasa na alikuwa ameshaomba ridhaa ya kuwa raia halali wa nchi
hiyo mwaka wa jana.
Wakati wa uvamizi huo, Amedy
Coulibaly,aliwaua watu wane wenye asili ya Uyahudi katika duka hilo
kubwa kabla hajapigwa risasi na polisi na kufa.


No comments:
Post a Comment