KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

January 27, 2015

LIPUMBA NA WANACHAMA 32 WA CUF WATIWA NGUVUNI LEO

Mwenyekiti wa CUF, Prof Ibrahimu Lipumba akizozana na polisi muda mfupi kabla ya kukamatwa pamoja na wafuasi wengine 32 wa chama hicho jijini Dar es Salaam. 


Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limewakamata wanachama wa Chama cha Wananchi CUF 32 akiwemo Mwenyekiti Taifa wa chama hicho,Profesa Ibrahim Lipumba kwa kufanya maandamano ambayo si halali.
Awali polisi ilizuia  maandamano yaliyokuwa yamepangwa na chama hicho ya  kuadhimisha kukumbuka ya miaka 14 tangu kufanyika kwa mauaji na mateso ya wananchi wa Zanzibar na Bara yalifanywa na vyombo vya usalama.
Akizungumza leo Naibu Kamishna wa Polisi Kanda ya Dar es Salaam,Simon Siro alisema wanachama waliokamatwa walikuwa 32 kati ya hao wawili ni wanawake na 30 ni wanaume ambao wote kwa pamoja wanashikiliwa na jeshi hilo kwa ajili ya mahojiano.
“Wanachama 32 akiwemo Profesa Lipumba tunawashikilia katika kituo cha Polisi Kati kwa kufanya maandamano ambayo hayana kibali, wote wapo hapa tunaendelea kuwahoji,”alisema Siro.
Siro alisema walipewa taarifa ya maandamano hayo na viongozi wa chama hicho hivyo jeshi hilo liliwaandikia barua ya kuzuia maandamano hayo kwa kuhofia fujo kutokea.
Siro alisema sababu kubwa ya kuzuia maandamano hayo yasifanyike kwa kuwa mwaka 2001 yalifanyika maandamano batili yaliyosababisha baadhi ya polisi na wananchi kufa.
“Jeshi la polisi likiruhusu hayo maandamano kuna uwezekano wa kutokea fujo na hayo maandamano ya mwaka 2001 yalikuwa si halali na kwenye maandamano hayo walikufa askari polisi,”alisema Siro.
Alisem sababu nyingine ya kuzuia maandamano hayo ni kuwa hivi karibuni walikamatwa watu wanaojihusisha na mambo ya ugaidi hivyo kutokana na mazingira hayo jeshi la polisi linazuia mikusanyiko mikubwa kwa kuhofia kutokea mambo mabaya.MWANANCHI

No comments:

Post a Comment