KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

January 27, 2015

MAMA WA MAPACHA SITA ALIYETELEKEZWA NA MUME WAKE AKABIDHIWA NYUMBA NA BENKI

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Covenant Bank Balozi, Salome Sijaona(Katikati) akikata utepe, kuashilia uzinduzi Rasmi wa nyumba aliyokabidhiwa Salome Mhando ambaye alitelekezwa na mume wake baada ya kujifungua watoto mapacha mfurulizo hadi kufikia sita na kukosa Mahali pa kuishi, Covenant Bank imemkabidhi nyumba hiyo ambayo ataimiliki yeye mwenyewe pamoja na thamani za ndani na Bima ya Matibabu kwa Mwaka mzima. Anaeshuhudia ni mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Sabetha Mwambenja (wa kwanza kushoto) na Salome Mhando (wa kwanza kulia).
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Covenant Bank Balozi, Salome Sijaona (kushoto), Pamoja na Mkurugenzi wa benki Hiyo, Sabetha Mwambenja, wakimkabidhi hati ya kiwanja na Umiliki wa nyumba Salome Mhando, Mama alietelekezwa na mume wake baada ya kujifungua watoto mapacha mfurulizo, hadi kufikia sita, Benki hiyo imemkabidhi nyumba hiyo pamoja na Bima ya Matibabu kwa mwaka mzima.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Covenant Bank Balozi, Salome Sijaona(Katikati) akiwapokea watoto wa Salome Mhando wakati akiwasili kukabidhiwa nyumba yake. Pamoja nae ni Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja na Mjumbe wa Bodi ya benki hiyo, Margaret Kyarwenda.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Covenant Bank Balozi, Salome Sijaona (wa kwanza kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja na Mama Salome Sijaona, Wakimfurahia moja wa watoto wa mama huyo akipanda katika moja ya vitanda walivyokabidhiwa.

No comments:

Post a Comment