![]() |
| Aaron Ramsey wa Arsenal akiwatoka wachezaji wa Manchester City, Jesus Navas (kulia) na Fernando (kushoto) wakati wa mtanange huo |
![]() |
| Kipa wa Arsenal, David Ospina akishangilia ushindi wa timu yake pamoja na beki wake Per Mertesacker (kulia). |
KLABU ya Manchester City imepokea kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa
Arsenal ikiwa nyumbani kwenye Uwanja wake wa Etihad jijini Manchester
leo.
Katika mechi hiyo ya Ligi Kuu ya England, mabao ya Arsenal yamewekwa
kimiani na Santi Cazorla kwa penalti huku la pili likifungwa na Olivier
Giroud kwa kichwa.
Kwa matokeo ya leo, Manchester City imeendelea kubaki nafasi ya pili
ikiwa na pointi 47 huku ikiwa na pointi 5 nyuma ya vinara wa ligi hiyo,
Chelsea wenye pointi 52. Asenal wapo nafasi ya tano wakiwa na pointi 39.








No comments:
Post a Comment