Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MKUU wa wilaya Temeke, DC Sophia Mjema, ameipongeza shule ya
Sekondari ya Kiislamu inayojulikana kama Twayyaibat Islamic Seminary Secondary
School kwa kufanya ada nafuu inayoweza kuwafanya wazazi na walezi wamudu
gharama za kusomesha watoto kwenye shule binafsi.
Mjema aliyasema hayo alipofanya ziara katika shule hiyo na
kukuta uongozi wa Twayyaibat, ukitoa ada ya Sh 200,000 tu kwa mwaka, jambo
ambalo ni agharabu mno hususan kwa shule za kulipia na zinazomilikiwa na
taasisi za kidini.
Akizungumza kwa mshangao mkubwa mbele ya wadau wa elimu, DC
Mjema alisema ameshangazwa na shule hiyo kufanya ada nafuu, hivyo ni jukumu la
wazazi na walezi kujitokeza kuwasomesha watoto wao kwa nguvu zote.
Mwanafunzi
kutoka Twayyibat Islamic Seminari akisoma Quraan katika shule hiyo
walipotembelewa na Mkuu wa Wilaya Temeke, Sofia Mjema, hayupo pichani.
Mkuu wa Wilaya Temeke, Sofia Mjema, kulia akimkabidhi cheti Mr Yakubu
kwa kutambua mchango wake kwa maendeleo ya shule ya Twayyibat Islamic
Seminary, iliyopo Temeke, jijini Dar es Salaam jana.


No comments:
Post a Comment