![]() |
| WAZIRI
wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, ameendelea na jitihada za
kutafuta ufumbuzi wa kudumu kuhusiana na changamoto zinazowakumba wadau
wa biashara ya utalii nchini. Katika kuhakikisha hilo linafanyika kwa mafanikio na kwa haraka, Nyalandu ametangaza kuanza kwa vikao vitakavyowakutanisha wataalamu wa Wizara zinazohusika na maliasili na utalii za Tanzania na Kenya kwa lengo la kujadiliana masuala mbalimbali iili yapatiwe ufumbuzi kwa maslahi ya pande zote. Hatua hiyo imetokana na hivi karibuni Serikali ya Kenya kuyazuia magari ya utalii kutoka Tanzania kuingiza watalii kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, hivyo kusababisha usumbufu mkubwa. Hata hivyo, Nyalandu aliingilia kati kwa kuzungumza na Waziri wa Utalii wa Kenya, Phillys Kandie na kufikiwa kwa makubaliano ya kuruhusiwa na hapo wazo wa wizara hizo kukutana likaibuliwa. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Nyalandu alisema vikao ya wataalamu hao vitaanza rasmi Februari 3, mwaka huu, jijini Arusha ambapo vitahusisha pia wataalamu kutoka Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Alisema vikao hivyo vitajadili masuala mbalimbali ili kuhakikisha changamoto zote zinawaikabili sekta ya utalii kwa nchi hizo mbili zinapatiwa ufumbuzi. |
January 25, 2015
NYALANDU NA CHANGAMOTO ZA UTALII NCHINI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment