![]() |
Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta akikagua Stesheni ya Reli Dar es Salaam jana alipotembelea mashirika na mamlaka zinazotoa huduma za uchukuzi . Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la (TRL), Elias Mshana. Picha na Venance Nestory |
Waziri Sitta ameanza rasmi majukumu mapya kwa
kupiga mkwara watumishi wa mashirika na taasisi zilizo chini ya wizara
yake na kutoa onyo kwa wahujumu na wezi wa rasilimali za umma.
Waziri Sitta alitangaza msimamo huo jana,
alipofanya ziara katika baadhi ya mashirika na kampuni zilizo chini ya
wizara yake, kwa lengo la kufahamu baadhi ya changamoto pamoja na
kuwahakikishia wafanyakazi utatuzi wa matatizo yao.
Waziri Sitta alitembelea na kuzungumza na
watendaji wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga, Mamlaka ya Reli ya Tazara,
Kampuni ya Reli (TRL) na pia akakutana na maofisa wa Kampuni ya Ndege
(ATCL) na aliwaeleza nia na hatua za Serikali kushughulikia changamoto
zinazowakabili kwa pamoja.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya
mazungumzo mafupi na watendaji wa TRL, Waziri Sitta alisema kazi zote
alizozianza mtangulizi wake katika wizara hiyo, Dk Harrison Mwakyembe
ataziendeleza tena kwa ukali zaidi na kusema si sahihi wezi wa kuku
wakachomwa moto huku wahujumu na wabadhirifu wakiachwa huru. MWANANCHI
No comments:
Post a Comment