………………………………………………………………..
Na Philemon Solomon
Na Philemon Solomon
Wakala wa Ukaguzi wa Madini
Tanzania(TMAA)umetoa wito kwa Umma kujiepusha na shughuli za utoroshaji
na biashara ya magendo ya madini kwani hatua kali zitaendelea
kuchukuliwa kwa yeyote atakaebainika kukutwa akijishughulisha na
utoroshaji wa madini.akiongea na waandishi wa habari leo Ofisini kwake
Mkurugenzi Utawala na Fedha Wakala wa Ukaguzi wa Madini
Tanzania(TMAA)Bw,Bruno Mteta.amesema
Moja ya majukumu ya wakala ni
kufuatilia na kuzuia utoroshaji magendo ya madini,na ukwepaji wa ulipaji
mrabaha kwa kushirikiana na vyombo na mamlaka nyingine husika za
serikali”katika kipindi cha kuanzia Septemba 2012 hadi Julai 2013,wakala
umeweza kukamata watoroshaji wa madini aina mbalambali katika matukio
23 tofauti ya madini yaliyokamatwa yana thamani ya jumla ya Dola za
Marekani 8,231,740,sawa na Shilingi za Kitanzania bilioni
13.17.watoroshaji hao walikamatwa na wakaguzi wa wakala waliopo katika
Madawati ya Ukaguzi wa Madini katika viwanja vya ndege vya Kimataifa vya
Dar es salaam,Kilimanjaro na Mwanza.watoroshaji hao walikamatwa na
wakaguzi wa Wakala kwa kushirikiana na Taasisi nyingine ambazo ni
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege(TMAA),Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA),Jeshi
la Polisi,Idara ya Uhamiaji na Usalama wa Taifa.watoroshaji hao wengi
wao ni raia wa kigeni na wachache ni Watanzania”alisem Mteta
Alitaja matukio ya hivi
karibuni,ambapo amesma”Tarehe 20 Agosti,2013,raia mmoja wa kigeni
alikamatwa na Mkaguzi wa Wakala kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere akiwa na aina mbalimbali ya madini ya vito yenye thamani
ya Dola za Marekani 15,826,sawa na Shilingi milioni 25.32.hatua za
kisheria zimechukuliwa dhidi yake ikiwa ni pamoja na kuyataifisha madini
hayo kuwa mali ya serikali.
Tarehe 20 Agosti,2013,raia mwingine wa kigeni alikamatwa na
Wakaguzi wa TMAA kwa kushirikiana na Askali Polisi,Usalama wa Taifa na
Ofisi ya Madini kanda ya Mashariki kwenye makazi ya huko Jangwani Beach
akiwa na aina mbalimbali ya madini ya vito.Uthaminishaji wa madini hayo
unaendelea,japokuwa yanaonekana kuwa na thamani kubwa sana.mtuhumiwa
anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi kwa uchungzi zaidi na hatua za
kisheria,vilevile unatoa wito kwa Umma kutoa taarifa kwa wakala pale
wanapobaini kuwepo kwa raia wa kigeni au Watanzania wanaojishughulisha
na utoroshaji au biashara haramu ya madini kwa mawasiliano ya
haraka,wananchi watumie barua pepe info@tmaa.go.tz na simu 022-2601819″alisema




No comments:
Post a Comment