![]()  | 
| Kaimu Kamanda Sirro. | 
 Jeshi
 La Polisi limetoa sababu za kwanini lilizuia maandano ya wafuasi na 
viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) kwamba ni kutokana na kuibwa kwa 
bunduki saba katika kituo cha Polisi Ikwiriri wilayani Rufiji, mkoani 
Pwani ambazo pengine zingeweza kutumika katika mkusanyiko wa watu.
Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro,
 akihojiwa jana na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) alisema 
jeshi hilo liliwasihi tangu awali viongozi wa CUF kwamba wasifanye 
maandamano kutokana na kuwapo kwa taarifa kuwa silaha zilizoibwa 
Ikwiriri zingetumika pengine katika maandamano hayo.
“Tuliwaeleza kuna silaha ambazo zimeibwa Ikwiriri na hatuwezi kujua
 zitatumika maeneo gani, lakini kuna uwezekano zikawa zimeingia Dar es 
Salaam, hivyo tukawaambia hizi silaha hatuwezi kujua zitapiga wapi na 
zitakuwa na madhara gani,” alisema Sirro.
Kamanda Sirro alisema sababu nyingine ambayo CUF walielezwa ni 
kwamba katika mauaji ambayo yalifanyika Pemba pia wapo askari polisi 
waliouawa, hivyo taarifa ambazo jeshi hilo lilikuwa limezipata ni kwamba
 maandamano hayo yasingeweza kwisha salama.
Juzi Jeshi la polisi lilitumia nguvu kwa kupiga mabomu na silaha za
 moto wakati wa kuwakamata wanachama wa CUF waliokuwa wamekusanyika 
baada ya jeshi hilo kuwazuia wasiandamane kufanya kumbukumbu ya 
wanachama wa chama hicho waliouawa na Jeshi hilo mwaka 2001.
     CHANZO:
     NIPASHE
    



No comments:
Post a Comment