Na Peter Fabian, MwanzaMKUU wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo, ambaye ni mwakilishi wa Rais Jakaya Kikwete mkoani hapa, amebuni aina mpya ya ulinzi wake binafsi pamoja na msafara wa magari unaoambatana naye anapokuwa katika ziara zake za kikazi.
Aina hiyo ya ulinzi na msafara wake wa magari unaofanana kwa kiwango kikubwa na ule wanaopewa viongozi wakuu wa kitaifa, akiwemo Rais na Waziri Mkuu, ni wa kwanza kushuhudiwa na wakazi wa mkoani hapa na umedaiwa kugharimu kiasi kikubwa cha fedha.
MTANZANIA Jumamosi limeushuhudia msafara huo unaowajumuisha pia askari wa usalama barabarani ambao kazi yao ni kujipanga barabarani na kuwazuia watumiaji wengine wa barabara wenye magari ili kusitisha kwanza safari zao mpaka hapo Mulongo na msafara wake wanapopita.
Katika msafara wake, Mulongo huambatana na Mkuu wa Polisi wa wilaya
husika, maofisa usalama wa wilaya na mkoa, magari kadhaa ya watumishi wa
Halmashauri ya Jiji la Mwanza pamoja na maofisa wa wilaya
anazozitembelea.
Sambamba na msafara huo wa magari, Mulongo pia analindwa na makundi matatu ya wanausalama ambao ni askari polisi wa kawaida, askari kanzu na maofisa usalama wa taifa.
Ingawa amekuwa akitumia aina hii ya ulinzi na usafiri hata katika safari zake za kawaida asubuhi anapotoka katika hoteli ya kitalii anayoishi kwenda ofisini wake, katika ziara yake ya kujitambulisha kwa wakazi wa Mkoa wa Mwanza aliyoianzia Wilaya ya Ilemela, ulinzi wake ulionekana kuimarishwa zaidi, huku idadi ya magari kwenye msafara wake nayo ikiongezeka.
Watu wa makundi mbalimbali waliozungumza na MTANZANIA Jumamosi kuhusu aina huyo mpya ya msafara na ulinzi wa Mulongo, wameeleza kushangazwa na jinsi mkuu huyo wa mkoa anavyojikweza na mwenendo wake wa kiuongozi waliodai kuwa una chembechembe za vitisho.
Wakizungumza kwa sharti la majina yao kutoandikwa gazetini kwa kile walichodai kuwa ni kuhofia kushughulikiwa na Mulongo, walisema wana mashaka na mwenendo wa kiongozi huyo na kubashiri kuwa unaweza kuwa na athari mbaya kwa serikali na hata Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Katika baadhi ya maeneo ambayo Mulongo alifika kujitambulisha na
kuzungumza na wananchi alionya kuwa serikali itawachukulia hatua wale
ambao wamekuwa wakijitokeza kwenda kulinda kura za wagombea wao nyakati
za uchaguzi.
“Nimekuja kwenu kujitambulisha kama Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, hilo ndilo lengo la ziara yangu hii ambayo ni ya kwanza tangu nifike mkoani hapa.
“Nataka mtambue kuwa jukumu lenu la kwanza ni kukomesha uhalifu, niwasihi toeni taarifa za uhalifu polisi. Lakini naambiwa na ninyi mna tabia ya kubeba mawe na silaha za jadi kwa madai ya kwenda kulinda kura katika maeneo ya vituo vya kupigia kura, sasa nawatahadharisha kuwa watakaobainika na kukamatwa watajuta na waliowatuma tutawashughulikia,” alionya Mulongo. MWANANCHI

No comments:
Post a Comment