![]() |
| Rais Kabila amekuwa mamlakani tangu mwaka 2001 |
Polisi
katika Jamuhuri ya kidemokrasi ya Congo, wamefyatua risasi hewani ili
kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wamekusanyika katika mji mkuu
Kinshasa kupinga sheria mpya ya uchaguzi.
Serikali inasema kuwa
watu wanne walifariki katika vurugu za Jumatatu ingawa upinzani unasema
idadi huo huenda ikwa kujuu kuliko iliyonakiliwa.Wanafunzi wameweka vizuizi barabarani na pia wameshuhjudiwa wakichoma magurudumu, katika barabara zinazoelekea katika chuo kikuu mjini humo.
Wanatuhumu wanasia wanaomuunga mkono Rais Joseph Kabila ambaye muhulka wake wa pili unatarajiwa kumalizika mwaka ujao kwa kujaribu kujiongeza muda mamlakani kwa kuidhinisha mipango ya kufanyika sensa ambayo itachelewesha uchaguzi kwa miaka mingi.
Vurugu hizi zinashuhudiwa huku baraza la Senate likidadisi mswada ambao huenda ukasababisha Rais Kabila kuongezwa muda mamlakani.



No comments:
Post a Comment