
Mwenyekiti
wa CUF, Prof Ibrahim Lipumba, akizungumza kwenye mkutano wa hadhara,
uliofanyika katika Viwanja vya Manzese Argentina, Dar es Salaam jana.
Picha na Emmanuel Herman
Siku tano baada ya kuzuiwa kufanya mkutano wa hadhara kwa madai ya tishio la ugaidi, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba jana alihutubia wananchi eneo la Manzese jijini Dar es Salaam bila kuwapo kwa ulinzi wa Jeshi la Polisi.
Mkutano
wa jana wa Profesa Lipumba, ambaye alijikuta kwenye matatizo na Jeshi la
Polisi baada ya kupigwa, kutiwa mbaroni na baadaye kufunguliwa mashtaka
Jumanne iliyopita, jana ulitawaliwa na amani na ulidumu kwa takriban
saa mbili kwenye eneo hilo la Manzese ambalo kwa kawaida huwa na utitiri
wa watu.
Profesa
Lipumba alikutwa na kadhia hiyo wakati akielekea Zakhem, Mbagala ambako
alidai kuwa alikuwa akienda kushawishi wananchi watawanyike kwa amani
baada ya Jeshi la Polisi kuzuia maandamano na mkutano wa hadhara.
Katika
tukio hilo, mwenyekiti huyo wa CUF alikamatwa pamoja na wafuasi 32 na
baadaye kufunguliwa mashtaka ya kula njama, kufanya maandamano na
kukusanyika bila ya kibali. Vitendo hivyo vya polisi vilisababisha Bunge
la Jamhuri ya Muungano kusitisha shughuli zake na kuamua kujadili tukio
hilo, bila ya kujali kuwa lilikuwa likiingilia shughuli za mhimili
mwingine wa nchi.(P.T)
Katika
mkutano wa jana, hakukuwa na polisi waliovalia sare kama ilivyo kawaida
kwenye mikutano ya hadhara ya kisiasa, hasa ya vyama vikubwa vya
upinzani, ambayo hulindwa na askari wenye silaha na jana jukumu hilo
lilifanywa na kikosi cha ulinzi cha chama hicho cha Blue Guards.
Alipotafutwa
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura alisema
hafahamu kuhusu suala hilo kwa kuwa yuko nje ya eneo lake la kazi.
"Hilo
silijui kwani nipo nje ya Dar es Salaam hivyo siwezi kulizungumzia,"
alisema Kamanda Wambura, ambaye alieleza kuwa yuko Dodoma ambako
kulikuwa na mkutano wa maofisa waandamizi wa Jeshi la Polisi
uliomalizika jana.SOMA ZAIDI CHANZO MWANANCHI


No comments:
Post a Comment