Marehemu, Mez B akiwa studio enzi za uhai wake.
ALIYEKUWA memba wa kundi la Chamber Squad, Moses Bushagama ‘Mez B’
ambaye amefariki jana mjini Dodoma anatarajiwa kuzikwa Jumatatu katika
makaburi ya Wahanga yaliopo Maili Mbili mjini Hapo. Mtandao huu uliongea
na mama wa marehemu, Marry Mkandawile ambaye alisema kuwa kwa sasa
msiba upo maeneo ya Kisasa mjini hapo.
UJUE UNDANI WA MEZ B
MSANII wa muziki wa Bongo Fleva aliyekuwa
akiwika na kundi la Chamber Squad, Moses Bushagama ‘Mez B’ amefariki
dunia asubuhi ya jan majira ya saa 4:30 mjini Dodoma.
Hii imekuwa ni pigo la pili kwa kundi la Chamber Squad kupoteza memba
wake baada ya awali kumpoteza Albert Mangweha ‘Ngwear’.Katika makala
haya yanauelezea undani wa Mez B mpaka kufikia umauti.


No comments:
Post a Comment