Na Mwandishi Wetu
Mfuko wa Umoja umeweza
kuwanufaisha Watanzania wengi na taasisi zilizowekeza kwa kutoa faida kubwa
tokea kuanzishwa kwake, Mfuko huu unaendeshwa na Dhamana ya Uwekezaji Tanzania ((UTT-AMIS) ambayo ni taasisi
iliyo chini ya Wizara ya Fedha iliyoanzishwa 2003.
Moja ya majukumu ya
Dhamana ni kuwawezesha Watanzania kushiriki katika masoko ya fedha, kuhamasisha
uwekaji wa akiba na kuendesha mifuko ya
uwekezaji wa pamoja kwa gharama nafuu .
Mkurugenzi wa Masoko wa
UTT-AMIS,Daud Mbaga, anasema kuwa Watanzania wanawezeshwa kwa kuweka
akiba kulingana na uwezo wao huku wakipata faida kutokana na uwekezaji kwenye
masoko ya mitaji na dhamana.
“Ili kuweza kushiriki
katika uwekezaji kupitia Dhamana mwekezaji anatakiwa kununua vipande ikiwa ni
sehemu ya umiliki wa mwekezaji kwenye mfuko husika,” anasema.
Anafafanua kuwa toka kuanzishwa kwake hadi
sasa Dhamana imeweza kuanzisha mifuko mitano (5) ambayo ni Umoja, Wekeza
Maisha, Jikimu, Watoto na Ukwasi.
“Watanzania wameweza
kujiunga kwenye mifuko inayoendeshwa na Dhamana ili kupata faida zitokanazo na
uwekezaji kwenye masoko ya mitaji na dhamana,”anafafanua.
Anasema Mfuko wa Umoja
ndio mfuko wa kwanza kuanzishwa na ulianza kuuza vipande mwezi Mei, 2005. Ni
mfuko wenye amana kubwa ambao kwenye mauzo ya mwanzo uliweza kukusanya zaidi ya
Shilingi bilioni 90 na kuvunja rekodi ya mauzo ya mwanzo (IPO) Afrika Mashariki
nzima.


No comments:
Post a Comment