Mkurugenzi
Mkuu Mstaafu wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa NHIF Mzee Emannuel Humba
akionyesha tuzo yake aliyopewa na mfuko huo kwa kutambua mchango wake
akiwa mwanzilishi wa mfuko huo wakati wa hafla ya kuwaaga viongozi na
wafanyakazi wastaafu iliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee
mwishoni mwa wiki , Mzee Emannuel Humba aliwaasa wafanyakazi wa mfuko
huo kushikamana na kufanya kazi kwa kujituma ili kuhakikisha mfuko huo
unafikia malengo, Katika hafla hiyo Emanuel Humba pia amezawadiwa zawadi
mbalimbali. wa pili kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi
ya NHIF Balozi Ali Mchumo na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo Bw. Michael Mhando.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE)
Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa NHIF akitoa shukurani zake kwa uongozi wa NHIF na wafanyakazi kwa ujumla kwa kuwaadalia hafla hiyo ya kuwaaga.
Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa NHIF akipokea shada la maua kutoka kwa Balozi Ali Mchumo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHIF.
Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti akizungumza katika hafla hiyo wakati akielezea wasifu wa baadhi viongozi wastaafu wa mfuko huo.


No comments:
Post a Comment