Na Andrew Chale wa modewji blog
Ikiwa ni siku moja tu tangu kutangazwa kwa wakuu wapya wa Wilaya
mbalimbali za Tanzania Bara, Uteuzi uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ikiwemo kumteua kada wa
Chama cha Mapinduzi anayetokea Jumuiya ya Vijana (UVCCM), Paul Makonda
kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, watanzania wengi wamebeza uteuzi huo
huku wengine wakiunga mkono.
Modewji blog iliweza kuongea na watu mbalimbali juu ya maoni yao kufuatia uteuzi huo wa Rais kwa kumchagua Makonda.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam baadhi ya
wasomaji wa mtandao huu, Sued Musa mkazi wa Kawe alibainisha kuwa,
uteuzi huo wa Rais ni mzuri ila alikosea kumweka wilaya ya kama
Kinondoni yenye matatizo chungu mzima ya kiutendaji ikiwemo migogoro ya
mipaka, ardhi, wafanyabiashara ndogondogo na mambo mengine ya ndani.
“Tunampongeza Rais kwa kuteua wakuu wapya wa mikoa, ila kwa huyu Paul
Makonda kumweka Kinondoni, ameteleza. Hii wilaya inahitaji mtu mwenye
uzoefu mkubwa katika uongozi na uadilifu” alisema Sued Musa.
Kwa upande wake, Jamal Tamba mkazi wa Kigogo, jijini Dar es Salaam,
alisema kuwa uteuzi huo ni mpya hivyo tuwape muda wateule wote wa Rais
na tutaona utendaji wao kama wanafaa ama lah!, alieleza.
Hata hivyo, kwa upande wa mitandao ya kijamii baadhi ya watu wameweza
kutoa maoni yao mbalimbali ambayo hata hivyo wengi wao wameyatoa kwa
kile wanachokijua wao ikiwemo masuala ya maslai ya kisiasa.


No comments:
Post a Comment