KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

March 28, 2015

KINANA:MAMA ANNE KILANGO MALECELA NI KATAPILLA LA SAME MASHARIKI, AMSIFU KWA KAZI NZURI

1
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Same Mashariki na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi mama Anne Kilango Malecela wakati alipowasili katika kijiji cha Maone akiwa katika ziara yake  ya Kikazi yenye lengo la kukagua na kuhimiza utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na kuhimiza uhai wa Chama Cha Mapinduzi CCM ambapo alikagua mradi wa chuo cha ufundi cha Maone na kumsifu mbunge wa jimbo hilo Mama Anne Kilango kuwa ni Katapilla kwa jinsi anavyowahangaikia wananchi wa jimbo la Same Mashariki. Chuo cha VETA Maone kitakapokamilika kitaweza kuchukua wanafunzi 300 kikichukua wanafunzi 180 wa kutwa na wengine 120 wa bweni na kitakuwa ni chuo pekee nchini kitakachoweza kutoa wanafunzi ambao wanaweza kujiunga na Chuo Kikuu moja kwa moja kutoka katika chuo hicho ambacho kitaendeshwa na  kitaendeshwa na Kanisa Katoliki Dayosisi ya Same. Katika ziara hiyo Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-SAME-KILIMANJARO)
11
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiponda kokoto wakati alipokagua ujenzi wa daraja la Mang’a Myamba Same Mashariki.
24
Blogger Ahmed Michuzi wa Jiachie ambaye ni mmoja wa wa mablogger ambao wapo katika  ziara hiyo akimpiga picha mama Anne Kilango aliyepakizwa kwenye pikipiki akielekea katika kiwanda cha kusindika  Tangawizi Myamba.
26
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia jinsi Tangawizi inavyosindikwa katika kiwanda hicho huku mkurugenzi wa SIDO Tanzania Bw.Omary Bakari akiangalia.
28
Wananchi wa NDugu wakifurahia jambo katika mkutano huo.
30
Naoe Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenyre kijiji cha Ndugu wilayani Same.                            

No comments:

Post a Comment