KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

March 28, 2015

MREMBO WA JAPAN WENYE ASILI AFRIKA AKUMBANA NA UBAGUZI WA RANGI

Miyamoto anasema  upinzani anaokutana nao ndiyo chachu itakayomfanya afanye vizuri kwenye mashindano ya Dunia ya  Miss Universe yatakayofanyika mapema mwakani.
Wengi katika eneo alilozaliwa la Nagasaki wanadhani kwamba mrembo huyo hapaswi kuwawakilisha katika mashindano mbalimbali ya urembo.
"Hapana,haonekani kama ni Mjapani, anasema Ishiko Komagawa.
"Mtu mchanganyiko siyo Mjapani kamili, Miss Japani anatakiwa wazazi wake wote wawe Wajapani, anasema Tomoki Nogami ambaye ni mwanafunzi
Akiwa amezaliwa na mama Mjapani na Baba Mwamerika Mweusi kutoka jimbo la Arkansas, Miyamoto wajapani wamwita "haafu" -- maana yake nusu -mjapani.
 "Watu wanakumbana na ubaguzi na chuku nchini Japan,anasema," Jeff Kingston, Profesa katika masomo ya Asia Chuo Kikuu cha Tokyo.
Anasema kumekuwa na watu wengi wenye vipaji katika michezo mbalimbali ambao wana asili mchanganyiko,ingawa Miyamoto amevunja minyororo katika eneo la urembo.

No comments:

Post a Comment