Ofisa Ugavi wa Manspaa ya Morogoro,
Vincent Odero kushoto akijadiliana jambo na Meneja miradi wa Selcom
Gallus Runyeta. kulia katikati ni Meneja Ukuzaji Biashara na Masoko, Juma Mgori na Afisa techinolojia habari na mawasiliano 'TEHAMA' wa Manspaa haiyo Innocent Cosma . Mheshimiwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro,Mkurugenzi Mama Theresia
Muhongo wageni waalikwa viongozi wa Halmashauri ya Mkoa wa Morogoro itifaki
imezingatiwa.
Awali ya yote kwanza kampuni ya Selcom inapenda kuwashukuru wote kwa jitihada
zenu binafsi kwa kuwezesha Jambo hili linalofanyika leo hii litimie. Safari hii
imeanza muda kidogo kuanzia kwenye mchakato wa tender hadi kufikia leo tuna
sign mkataba kwa kweli kwanza tunapenda kumshukuru Mungu kwani ni yeye ndo
ametuwezesha sote tufike hapa tulipofika leo. Na pia tunatoa shukrani zetu za
dhati kwenu wote kwa kuonesha Imani kubwa kwetu sisi Selcom. Na tunawaahidi
hatutawangusha hata kidogo tunapenda kuwajulisha kuwa chaguo lenu kwetu ni
sahihi kabisa na hamtajutia hilo.
Baada ya neno hilo la shukrani napenda kidogo kueleza sisi Selcom ni nani?
Selcom ni kampuni ya kizawa na inayomilikiwa na Wazawa tena wazalendo na
ilianzishwa mwaka 2001, na kuanzia kuanzishwa kwake tumejikita kwenye nyanja ya
urahisishaji wa mifumo ya malipo kwa njia ya kieletroniki. Selcom ndiyo muuzaji
namba moja wa mauzo yote ya LUKU nchini na mafanikio haya yamepatikana kutokana
na ubora wa hali ya juu wa mifumo yetu. Selcom hivi sasa inajivunia kuwa na
mawakala zaidi ya 8,000 nchini kote ambao wanatoa huduma kwa kutumia PoS zetu.
Mbali ya PoS kampuni yetu ndiyo inaongoza nchini kwa kuunganisha huduma zake
kwenye zaidi ya mabenki 30 nchini ambayo nayo yamerahisisha wateja wake kufanya
manunuzi mbalimbali na hata malipo kwa kupitia mtandao wetu.
Mbali ya mabenki hayo 30 ambayo yanatumia mtandao wetu, Selcom pia inawezesha
makampuni ya Tigo Pesa, Airtel Money na Mpesa kufanya manunuzi ya huduma ya
LUKU. Hivyo mtumiaji wa simu anaponunua LUKU kutumia simu yake basi atambue
anatumia huduma zetu.
Katika jitihada za kuwakwamua Watanzania hususani inapokuja kwenye suala la
malipo hatukuishia hapo. Hivi karibuni Selcom tumezindua huduma zetu mpya za
ATM na Selcom card chini ya brand ya Selcom Cashpoint na Selcom Paypoint.
Kwenye ATM zetu mteja wetu ataweza kufanya miamala yote ya simu kwa mitandao
yote pasipo usumbufu na kwa haraka na kwa kupitia card zetu mteja ataweza fanya
malipo yote na pia kufanya miamala kwa kutoa au kutuma pesa kwenye mitandao
yote.
Kama Selcom, hatukuishia hapo kupitia benki 30 ambazo zimeungana na mtandao
wetu mteja, mbali ya kufanya manunuzi na malipo ya huduma mbalimbali ataweza
kufanya miamala ya kutuma pesa, kuhamisha pesa bila kujali kama ni kutoka
kwenye simu yake kwenda benki au kutoka benki kwenda kwenye simu yake.
Huduma zetu zimekuwa zikikuwa kwa kasi na idadi kubwa sasa ya Watanzania
wamekuwa wakizitumia kila kukicha. Takwimu zinaonesha zaidi ya Watumiaji LAKI
SITA wamekuwa wakitumia huduma zetu kila Siku hii ni kwa kufanya manunuzi au
malipo mbalimbali na hii ni Baraka kubwa kwetu na ni kutokana na ubora na
umahiri wa mtandao wetu.
Mtandao wetu umekuwa bora na ukitegemewa na wengi kutokana na ubora wake na
kwamba Teknolojia iliyotumika imetengenezwa nchini na unaratibiwa hapa hapa
nchini na Wataalamu ambao ni Watanzania wazalendo bila kutegemea kitu chochote
kutoka nje. Na hii ndo Siri kubwa ya mafanikio yetu Selcom.
Leo kwa ushirikiano na Halmashauri ya Morogoro tunasaini mkataba ambao utaleta
mapinduzi makubwa katika ukusanyaji wa Mapato kwa njia za kieletroniki. Tukiwa
na Imani kwamba mifumo yetu ya ukusanyaji wa malipo itaiwezesha Halmashauri ya
Morogoro kuongeza pato lake maradufu. Tunaanza na ukusanyaji wa kodi za
Majengo, mabango, soko la Mawenzi, hospitali na zanahati za afya.
Huduma rasmi ya malipo kwenye sehemu zilizotajwa itaanza rasmi tarehe 1 ya
mwezi Aprili. Kwa sasa hivi tutakuwa kwenye kipindi cha majaribio ambayo kwa
kiasi Kiikubwa yatahusisha sehemu husika zilizotajwa.
Kwa wakazi wa Morogoro, Selcom imekuletea ajira mlangoni kwako kwa kuongeza
fursa ya wewe kuwa wakala wetu na mjasiliamali ambaye utahusika moja kwa moja
katika kusaidia makusanyo ya kodi na hapo hapo kujiongezea kipato. Kwa maelezo
ya jinsi ya kuwa wakala wetu, tafadhali fika ofisini kwetu Mtaa wa Jamhuri au
kwa kutupigia simu namba 0784 670 075 au wasiliana moja na moja na Aly Mbaga
kwa simu namba 0719 325 335.
|
No comments:
Post a Comment