KIWANGO cha mvua katika msimu wa mwaka huu wa masika
ni kidogo kwenye maeneo mengi ya nchi hali inayoweza kusababisha ukame
endapo Watanzania hawatazitumia kwa busara mvua chache zinazotarajiwa
kunyesha nchini. Utabiri wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), juu
ya mwelekeo wa mvua kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia sasa, ulisema
licha ya maeneo mengi ya nchi kutarajia mvua za wastani, maeneo mengine
mvua zitakuwa kubwa. Baadhi ya maeneo hayo ni kanda ya Ziwa Viktoria,
mikoa ya Kagera, Simiyu na mikoa ya kusini mwa nchi ukiwemo Lindi,
Ruvuma, Mtwara na Mashariki mwa mkoa wa Mbeya. Akizungumza na waandishi
wa habari ofisi za TMA, Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa wa
Mamlaka hiyo, Dk. Agnes Kijazi, alisema kwa mwaka huu masika inakuja na
mvua chache kutokana na mabadiliko ya tabia nchi. Dk. Agnes alisema pia
licha ya mabadiliko hayo, ambayo wengi walitarajia unafuu wa hali ya
hewa katika kipindi hiki ambacho maeneo mengi likiwemo jiji la Dar es
Salaam joto limekuwa juu.UHURU
No comments:
Post a Comment