KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

March 30, 2015

WASAMBAZA PICHA ZA NGONO SOMENI HII: MTAKWENDA JELA MIAKA SABA,WAZUSHI NA NINYI MTAKULA MIEZI SITA JELA!

Leo serikali itawasilisha Muswada wa Sheria ya makosa ya Mtandao wa mwaka 2015 hati ya dharura unaoorodhesa adhabu mbalimbali, ikiwamo ya faini ya sh50 milioni au kifungo kisichopungua miaka saba kwa mtu atakayebainika kusambaza picha  za ngono mtandaoni.

Baadhi ya makosa yaliyoainishwa katika sheria hiyo ni kutuma taarifa bila ridhaa ya mtu, kusambaza picha za ngono za utupu unaohusiana na kompyuta, makosa yanayohusiana na utambuzi kughushi kunakohusiana na masuala ya kompyuta na kusambaza picha za utupu za watoto......

 Inawabana pia watoa taarifa a uongo,katika kifungu 16 inasema mtu atakayetoa taarifa takwimu au maelezo kwa njia ya picha au maandishi au aina nyingine yoyote ikiwa ni za uongo akipatikana na hatia atalipa faini isiyopungua shilingi  milioni tatu au kifufungo kisihopungua miezi sita.

No comments:

Post a Comment