KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

April 19, 2015

KINANA ASHIRIKI KATIKA BONANZA LA VILABU VYA JOGGING MKOA WA DAR ES SALAAM, VIJANA WATAKIWA KUJIANDIKISHA DAFTARI LA WAPIGA KURA

k01
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akianza mazoezi wakati akishiriki  katika bonanza la Jogging lililoandaliwa na Kundi la Kaza Moyo Jogging Club la Ukonga Sitakishari ili kuhamasishwa vijana kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura . Mazoezi hayo yameanzia katika viwanja vya Gonga Gongo la Mboto kupitia Kipawa  na kuishia kwenye uwanja wa Social Sitaki Shari Ukonga ujumbe mkuu wa Bonanza hilo ulikuwa ni kuwataka vijana kujitokeza kwa wingi kujiandikisha ili kupata haki ya kupiga kura kuliko kuwa mashabiki tu, Bonanza hilo la mazoezi limeshirikisha vilabu mbalimbali vya Joging kutoka mkoa wa Dar es salaam, Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Mogo George Shinga Mtambalike, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Ramadhan Madabida na kulia ni Bona Kaluwa Diwani wa Kata ya Kipawa
k11
Kinana akifurahia jambo na watoto katika mazoezi hayo huku Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Ndugu Ramadhan Madabida kulia akimuangalia.
k19
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akiongoza Mazoezi hayo kwenye uwanja wa Social Sitaki Shari Ukonga.
k29
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipiga picha na pamoja na vijana wa klabu ya Kaza Moyo Jogging Club mara baada ya kushiriki katika bonanza lao, Kulia ni Bona Kaluwa Diwani wa Kata ya Kipawa na kushoto ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mogo Ndugu George Mtambalike.
k30
Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari wakati alipotoa wito kwa tume ya uchaguzi kuhakikisha wanawahamasisha vijana ili kuiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura                               

No comments:

Post a Comment