![]() | ||||||
| Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akishiriki ibada ya pasaka na waumini wa kanisa la RC Mavanga jimboni kwake.
MBUNGE wa
Ludewa Deo
Filikunjombe aipongeza tume ya taifa ya uchaguzi (NEC) Kwa kusogeza
mbele zoezi la upigaji kura za maoni kwa katiba inayopendekezwa na
kuwa hatua iliyofikiwa katika mchakato huo ni kubwa na kumbukumbu
kubwa kwa Rais Jakaya Kikwete anapoondoka madakarani na urithi kwa Rais
ajaye kuendeleza mchakato huo.
Filikunjombe alitoa pongezi hizo wakati akitoa salamu zake za pasaka jana kwa waumini wa madhehebu mbali mbali ya Kikristo
katika wilaya ya
Ludewa salam zilizoambatana na
msaada wa viti ,bati ,vinada na saruji katika
makanisa hayo kama moja ya utekelezaji wa ahadi
zake kwa madhehebu hayo kama ambavyo walivyomuomba .
Alisema
kuwa hatua ya tume ya taifa ya uchaguzi kuongeza muda katika zoezi
hilo la kura za maoni kwa katiba inayopendekezwa mbali
yakuwapunguzia majukumu watanzania ya kufanya mambo mengi kwa wakati
mmoja bado kusogezwa huko mbele kutawafanya watanzania hasa wananchi
wake wa ludewa kuendelea na shughuli nyingine za uzalishaji mali.
'hakuna
uharaka wa kuharakisha zoezi la upigaji kura za maoni katika
katiba inayopendekezwa kwani hadi sasa hatua iliyofikiwa ni nzuri na
kumbukumbu kubwa kwa rais Jakaya kikwete anapomaliza muda wake kuwa
amefanya jambo hilo kubwa hadi lilipoishia na Rais ajaye ataanzia
alipoishia kikwete kwa kukamilisha katiba hiyo kuliko kukimbizana
kama ilivyopangwa awali kabla ya tume kusogeza mbele zoezi hilo kwa
muda usiofahamika'
| . | . |
April 6, 2015
FILIKUNJOMBE AIFAGILIA NEC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment