![]() |
| Maandamano Garissa |
Wananchi wa mji wa Garissa nchini Kenya wamefanya maandamano kupinga
vitendo vya kundi la Al Shabaab, lililoshambulia chuo kimoja kikuu mjini
humo na kuwaua watu 147 wengi wao wakiwa wanafunzi hapo jana.
Waandamanaji
pia wameelezea kutoridhika na vyombo vya usalama nchini humo wakisema
havikuchukua hatua za kutosha kutoa ulinzi kwa waliouawa na kwa raia
wengine kwa jumla.Wazazi, jamaa na marafiki wa wanafunzi waliouawa katika chuo kikuu cha Garissa wamekuwa wakiendelea kuwasili katika eneo hilo kuitambua miili ya wapendwa wao.
Waliojeruhiwa wanaendelea kupata matibabu .



No comments:
Post a Comment