Akitoa mahubiri kwa mamia ya waumini wa kanisa
hilo jana, Gwajima alisema ajali nyingi si za kawaida, bali ni makafara
yanayotolewa na baadhi ya watu na kutaka kila mmoja kuliombea Taifa ili
kuondokana na tatizo hilo.
Gwajima ambaye anatuhumiwa kwa kuachia silaha
katika mikono isiyo salama pamoja na kumkashifu, Askofu Mkuu wa Kanisa
Katoliki Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, alisema takwimu za Kikosi
cha Usalama Barabarani zinaonyesha kwamba tangu Januari hadi Machi,
mwaka huu, watu 866 walikufa kwa ajali za barabarani na wengine 2,370
kujeruhiwa.
“Ni lazima tujiulize ni kwa nini watu wengi
wamekufa kwa ajali mwaka huu, haya ni makafara yanayotolewa na watu,
naomba makafara yawarudie wenyewe waliyoyatengeneza,” alisema bila
kutaja majina.
Alisema idadi ya watu waliokufa ni ya kuishia Machi na kwamba idadi ya Aprili ikiongezwa, itaongezeka karibu mara mbili.
Katika takwimmu za Gazeti hili, kwa mwezi Aprili pekee, ajali zilizoripotiwa zimeua watu 104 hadi kufikia Aprili 17.
Gwajima alisema kuna sababu nyingi ambazo zimekuwa
zikitolewa kuwa zinasababisha ajali za barabarani na kwamba Serikali
inatakiwa kutafakari kwa kina.
“Wanasema ajali zinasababishwa na madereva walevi,
kwani miaka iliyopita hakukuwa na walevi, wanasema madereva hawana
mikataba ya ajira, mwaka jana walikuwa nayo hiyo mikataba, tujiulize kwa
nini sasa?” alisema.
No comments:
Post a Comment