Bondia wa ngumi za kulipwa, Mohammed
Matumla. IMEFAHAMIKA kuwa ile safari ya bondia wa ngumi za kulipwa,
Mohammed Matumla kwenda kuzichapa katika pambano la utangulizi
litakalowakutanisha mabondia Floyd Mayweather Jr dhidi ya Manny Pacquiao
nchini Marekani, Mei 2, mwaka huu, inaweza kuwa imeishia kwenye Ukumbi
wa Diamond Jubilee, Dar.Matumla alipata nafasi hiyo baada ya kumchapa
kwa pointi Wang Xin Hua wa China katika pambano la Ubingwa wa Dunia wa
WBF ambapo ilielezwa mshindi atasafiri mpaka Marekani kwa ajii ya
pambano hilo.Taarifa za uhakika ni kuwa ratiba ya mabondia watakaopanda
ulingoni siku hiyo imeshatolewa bila ya kuwepo kwa jina la Mtanzania
huyo.Akizungumza na Championi Ijumaa, Mohammed alisema: “Sioni kama kuna
dalili za kwenda kupigana huko Marekani kwa sababu promota amekuwa
haeleweki na kila ninapofanya mawasiliano naye anasema wanasubiria
majibu ya video walizotuma napigana na Mchina.“Makubaliano hayakuwa
hivyo kwani wao walisema mshindi atakwenda Marekani, hata maandalizi
bado sijaanza, unadhani kuna nini hapo?”Juzi, promota aliyesimamia
pambano la Mohammed, Jay Msangi alipotafutwa alisema: “Niko bize naongea
kwenye Skype na Rais wa WBF, Howard Golgberd kuhusu ripoti ya Mommed
Matumla ambapo atakuwa na majibu, nitafute kesho (jana).” Alipotafutwa
jana Alhamisi hakupokea simu.
|
April 6, 2015
SAFARI YA MATUMLA YA MAREKANI YAISHIA DIAMOND JUBILEE,PROMOTA ALALA MBELE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment