KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

April 27, 2015

UGAWAJI VYETI VYA URAIA KWA WATZ WAPYA 152,572 WAFIKIA UKINGONI

1
Afisa Uhakiki, Neema Chilipweli (kushoto) akiihakiki familia ya Yohanna Bukuru (watatu kulia), pamoja na mkewe na watoto wao sita kutoka Kijiji cha Kapemba, Kata ya Mishamo, wilayani Mpanda Vijijini, Mkoa wa Katavi, ikiwa ni hatua ya awali ya uhakiki ili familia hiyo iweze kupewa vyeti vya uraia wa Tanzania. Zaidi ya watu 152,572 katika Makazi ya Mishamo, Katumba na Ulyankulu waliokuwa wakimbizi wa Burundi wa mwaka 1972 walioomba uraia 2008 na kupewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi mwaka 2010, wanastahili kupokea vyeti hivyo kama raia wapya wa Tanzania. Hata hivyo, Makazi ya Katumba na Ulyakulu tayari wamekamilisha zoezi la ugawaji wa vyeti hivyo, na sasa ni zamu ya raia wapya wa Makazi ya Mishamo ambapo wiki hii zoezi la ugawaji wa vyeti hivyo nchini, linatarajiwa kukamilika. Serikali ya Tanzania inashirikiana na Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR) katika ugawaji wa vyeti hiyo.

No comments:

Post a Comment